Ni gari la polisi au Rais lililoibiwa Kenya?
Msemaji wa serikali amekanusha madai kuwa gari lililoibiwa lilikuwa la ulinzi wa Rais aarifa za kutatanisha za kuibiwa kwa gari la ulinzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta zimeibuka nchini humo. Taarifa hii ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari ingawa msemaji wa Rais Kenyatta ameikanusha taarifa hiyo akisema kuwa gari lililoibiwa lilikuwa la idara ya polisi likiendeshwa na inspekta mkuu wa polisi. Gari hilo lililokuwa lisemekana kuwa na uwezo wa kuhimili risasi, liliibiwa usiku wa Jumatano na kwamba aliyekuwa analiendesha gari hilo alikuwa afisa wa polisi. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Daily Nation ikimnukuu mtu anayesemekana kuwa dereva wa gari hilo la kifahari alilazimishwa kuvua nguo zake kabla ya kupokonywa gari hillo. Gari lenyewe lilikuwa na nambari ya usajili ya kibinafsi. Ni gari la polisi au la Rais? ...