COUTINHO AACHA HISTORIA ZANZIBAR
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil anayekipiga kwenye klabu ya soka ya Yanga ameonyesha kuwa yeye hakuja nchini kuuza sura na akiendelea kudhihirisha kuwa yeye ni Mbrazil kweli baaada ya kuiwezesha klabu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa tatu mfululizo visiwani Zanzibar.
Coutinho alikuwa miongoni mwa wafungaji katika ushindi wa mabao 2-0 Yanga waliopata dhidi ya KMKM kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar.
Akicheza kwa kujiamini na kiufundi mkubwa Coutinho alifunga bao la kwanza na la pili tangu atue nchini kwenye dakika 43 ya mchezo, bao hilo la Coutinho liliibua shangwe kubwa kwa mashabiki waliofurika uwanjani ambao walionekana kufurahishwa zaidi na uwezo wa mchezaji huyo wa Kibrazil.
kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko ya kikosi chao chote ikiwa sehemu ya majaribio ya wachezaji iliyowekwa na kocha Marcio Maximo katika maandalizi ya timu yake. mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda kwa Yanga waliotawala mchezo kwa asilimia kubwa baada ya mshambuliji wao Hussein Javu kupigilia msumari wa pili.
Akiongea na MWAISABULA BLOGU Coutinho alisema anajisikiio faraja kuona amekuwa miongoni mwa watu walioiwezesha klabu kuibuka na ushindi huku akishukuru kwa ushirikiano anaoupata kwa mashabiki wa klabu hiyo.
"nashukuru Mungu tumepata tena ushindi na mimi nikifunga moja, nitoe shukrani kwa mashabiki wa klabu hii kwa ushirikiano ninaoupata kutoka kwao" alisema Coutinho.
JAJA AKISALIMIANA NA MASHABIKI KWENYE UWANJA WA AMAAN
MRISHO NGASSA AKINYWA MAJI BAADA YA USHINDI
DEOGRATIOUS MUNISHI 'DIDA' AKIWA KWENYE POZI BAADA YA MECHI -Mwaisabula
Maoni
Chapisha Maoni