Shakira Atuhumiwa Kuiba Wimbo
Wimbo uliovuma wa mwimbaji wa
Pop Shakira ulinakiliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa kazi
ya mtungaji mwingine wa nyimbo, jaji mmoja mjini New York amegundua.
Jaji Alvin Hellerstein alisema toleo la wimbo
“Loca” la lugha ya kihispania 2010 lilikiuka haki za umiliki za wimbo wa
mwimbaji Ramon Arias Vazquez.Toleo la Ramon la “Loca” kwa lugha ya kiingereza- lililotumika katika Dizzee Rascal – “halikutolewa kama ushahidi,” katika kusikizwa kwa kesi hiyo.
Hakuna toleo lolote kati ya matoleo hayo mawili lililotolewa Uingereza.
Hata hivyo, toleo la kihispania – linalomshirikisha Eduard Edwin Bello Pou, anayefahamika kama El Cata – lilitolewa na kuvuma kote ulimwenguni na kuuza zaidi ya kanda milioni tano na kuongoza kwenye chati za kilatino kwenye Billboard Magazine.
Aidha, wimbo huo ulikuwemo kwenye albamu yake ya 2010 ‘Sale el Sol’ iliyouzwa kwa wasikilizaji wa Kiingereza na mada ya “The Sun Comes Out,” na matoleo yote mawili ya wimbo huo yalikuwemo.
Katika uamuzi uliotolewa Jumanne, jaji Hellerstein alisema kuwa, japo wimbo huo ulikuwa umetungwa ukifuata wimbo uliokuwa umerekodiwa hapo awali na Bello [El Cata], pia ulikuwa umenakiliwa kutoka kwa wimbo mwingine wa Arias Vasquez.
"Hakuna shaka kuwa toleo la Shakira la wimbo huo lilitungwa likifuata toleo la hapo awali la Bello,” jaji huyo aliandika kwenye uamuzi wake.
"Kwa hiyo, nimepata kuwa, kwa kuwa Bello alinakili Arias, yeyote aliyeandika toleo la Shakira pia alinaliki kwa njia isiyo ya moja kwa moja Arias,” alikata kauli.
Ramon Arias Vazquez alitunga wimbo Loca con su Tiguere miaka ya 1990, lakini Bello amekana kuunakili wimbo huo.
Uamuzi unatarajiwa kuelekeza fidia atakayolipwa mlalamikaji Mayimba Music, mmiliki wa haki miliki za hati ya Aria.
Sony ilisambaza matoleo yote mawili ya wimbo wa Shakira, toleo la Kiingereza, na la Kihispania, lakini tuhuma zilizotolewa ziliangazia toleo la kihispania.
Tarehe 13 Julai, Shakira, mwimbaji wa Colombia, alitumbuiza umati na wimbo huo katika sherehe ya kuhitimisha kombe la Dunia huko Rio de Janeiro.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni