KOCHA Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, ameamua kubadili kikosi chake ili aweze kuifanyia kitu mbaya Azam FC katika mchezo utakaozikutanisha timu hizo wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Goran Kopunovic Simba na Azam zitapambana Jumapili kuwania kuweka sawa mipango ya kushika nafasi ya pili, ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani. Azam wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 45, Simba wakiwa nyuma yao katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 41, wakibakiwa na michezo miwili, huku wakiwaombea mabaya Wanalambalamba hao wapoteze michezo yao mitatu ili wawapiku. Kama Simba watashinda michezo yao hiyo miwili dhidi ya Azam na JKT Ruvu na Wanalambalamba hao wakafanya vibaya michezo yao, ikiwamo huo wa Simba, Yanga pamoja na Mgambo JKT itawapa fursa ya kumaliza nafasi ya pili. Kutokana na hali hiyo, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, ameanza kuzichanga vema karata