ZIJUE FAIDA ZA KUSOMA NJE YA NCHI
ASILIMIA kubwa ya Watanzania hupenda kwenda kusoma nje ya nchi jambo ambalo linaonekana kuwa ni la kawaida sasa. Hulka hii inatokana na ukweli kwamba fursa za kusoma katika nchi nyingine zinaweza kumfaidisha mwanafunzi pindi atakapofika katika nchi husika. Wanafunzi wanafursa ya kusoma katika nchi ya kigeni na kuona utamaduni na desturi za mazingira tofauti uliyoyazoea maishani mwao. Sababu muhimu ambazo zinaweza zikakufanya kwenda kusoma nje: Kuiona dunia Sababu kubwa unapaswa kufikiria kusoma nje ni fursa ya kuona dunia kwa maana kuwa ndani ya sayari ya dunia zipo nchi nyingi hivyo nafasi ya kusafiri kutoka nchi moja hadi nyingine ni fursa muhimu kwa binadamu yeyote kujifunza mapya tofauti na nchi aliyotoka. Hii itamsaidia pia kuchangamana na watu wenye mitazamo na desturi mpya. Lakini pia mbali ya kufaidi mazingira ya nchi unayojipatia elimu pia upo uwezekano wa kusafiri au kutembelea maeneo mengine wakati wa masomo yako, unaweza pia kutembelea nchi za jirani. El...