Changamkieni uwanja huu mpige fedha
Na FARAJA MASINDE
DUNIANI kote klabu mbalimbali za soka
zinachangamkia jukwaa la mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwafikia kwa
haraka na kwa ukaribu zaidi mashabiki wao walioko kila pembe ya dunia.
Ni
wazi kuwa klabu hizi, hususan za barani Ulaya zinafanikiwa kwa kiwango
kikubwa kuiona fursa hii ya kiteknolojia inayoletwa na mitandao ya
kijamii ili kuwasaidia kutengeneza mapato na kuongeza mashabiki.
Mifano
mizuri kwenye hili ni pamoja na vilabu vikubwa kama, Arsenal, Chelsea,
Bayern Munich, Barcelona, Real Madrid ambazo zimekuwa zikiitumia vilivyo
mitandao ya kijamii katika kupata mafanikio.
Ukiacha
klabu zenyewe kwa ujumla, lakini pia kumekuwa na mitandao binafsi
ambayo imekuwa ikiingia mikataba na wachezaji binafsi ili kukuza thamani
zao na wao pia kunufaika, jambo ambalo limechochea uzito wa majina ya
baadhi ya mastaa.
Miongoni mwa tovuti hizo
ni pamoja na ile ya Dugout.com, ambayo ina jumla ya wachezaji 150
duniani, wakiwamo Gareth Bale, Alexis Sanchez, Edinson Cavani, Joe Hart
na Neymar JR.
Inafahamika kwamba, kwasasa
si tu kwamba mashabiki wanahitaji kuona wachezaji wakiwa uwanjani,
lakini pia hata kupata taarifa zao wakiwa nje ya uwanja ni jambo ambalo
limekuwa likipendwa na mashabiki wengi wa soka duniani.
Kwani
wamekuwa wakipenda kujua maisha ya mchezaji nje na ndani ya uwanja,
ikiwamo pia mahojiano mbalimbali ya mchezaji ambayo mara nyingi yamekuwa
yakipatikana kwenye tovuti ya klabu au hata kwenye ukurasa binafsi wa
mchezaji mtandaoni.
Tukirejea nyumbani
Bongo, bado utakuta ni Simba na Azam ambazo tovuti zake zipo hai,
tofauti na klabu nyingine ambazo zina tovuti ‘jina’, kwani zimekuwa
hazina taarifa zozote mpya na kufanya kudorora.
Kwani
klabu inapokuwa na tovuti ambayo iko hai inakuwa ni rahisi hata
kushawishi makampuni kuweza kutumia tovuti hizo, jambo ambalo linakuwa
na manufaa kwa klabu husika.
Ukiacha hilo,
lakini pia kwa mchezaji binafsi anaweza kunafaika kwa kutumia mitandao
hii ya kijamii katika kuweka taarifa zake na mambo mengine amb
Maoni
Chapisha Maoni