Miaka 30 jela kwa kuoa binti wa miaka minane
MKAZI wa Kijiji cha Nyaburundu wilayani Bunda, Changwe Changige (54), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumuoa na kumbaka binti mwenye umri wa miaka minane. Pia baba mzazi wa binti huyo ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, Kakwa Runguya (53), naye amehukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la udhalilishaji kwa kumuoza binti yake kwa mwanamume huyo. Mahakama ya Wilaya ya Bunda ilidai kuwa baba huyo amehukumiwa kutumikia kifungo hicho kwa kumuoza binti yake na kumnyima fursa ya kusoma. Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Hamza Mdogwa, alidai kuwa washtakiwa wote wawili walitenda makosa hayo Januari Mosi, mwaka jana saa 10 jioni katika kijiji hicho. Mdogwa alidai kuwa washtakiwa wote wawili walishtakiwa kwa kosa la kwanza ambalo ni kula njama na kumuoza binti huyo huku Changwe aliyemuoa na kumbaka binti huyo alishtakiwa kwa kosa la pili la ubakaji na Kakwa alishtakiwa kwa kosa lingine la udhalilishaji. Akitoa hukumu hiyo, H...