Mradi wa kusaidia wajasiria mali wanake wazinduliwa Dar
TAASISI
isiyo ya kiserikali ya Africanm Women and Beyond (WAB), kutoka nchini
Kenya, imefanya uzinduzi wa mradi maalum wa kusaka
wajasiriamali wanawake wa Tanzania ambao watapata fursa ya kupewa elimu,
kutafutiwa masoko na kuunganishwa na wanawake waliofanikiwa zaidi barani Afrika, ili kukuza biashara zao.
Uzinduzi huo
umefanyika katika viwanja vya Mnazimmoja, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza,
Dar es Salaam, jana, Mkurugenzi WAB, Joe
Kairuki, alisema kupitia mradi huo,
wataandikisha wajasiriamali 10,000 ambao watakwenda nchini Kenya, kushiriki mafunzo
mbalimbali ya kukuza biashara zao.
“Mapema
mwakani tutafanya mkutano mkubwa wa wajasiriamali, nchini Kenya, ambapo
tunatarajia, wanawake matajiri na watoto wa viongozi mbalimbali kuhudhuria, wakiwemo
Susane Owiyo na Tabitha Karanja ambao ni miongoni mwa
wanawake matajiri nchini Kenya,
Dk. Hafsat Abiola , Lindo Mandela
ambaye ni mkwe wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela na Melte
Knudsen ambaye ni Balozi wa Denmark
nchini Kenya,”alisema Kairuki.
Alibainisha
kuwa, wameamua kutafuta wajasiria mali nchini Tanzania, kutokana na kutambua
uhusiano muhimu uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuendeleza ushirika wa
Afrika Mashariki.
“Vigezo
vyetu ni mwanamke yoyote mhjjasiria mali, bila kujari ukubwa wa pato lake au
biashara yake. Tunawaomba wanawake
kujitokeza kwa wingi kesho (leo) ambapo tutaanza uandikishaji, viwanja vya
Mnanazimmoja,”alisema Kairuki.
Naye mmoja
wa waratibu wa mradi huo, Martine Kappel, alisema kuwa, mradi huo unalenga kuwakomboa wanawake barani Afrika.
“WAB inaamini
kuwa, kumkomboa mwanamke ni kulikomboa taifa lolote duniani. Kupitia mradi huu
tunaamini kwamba, wanawake wengi watakuza biashara zao kwa kuunganisha soko na watu waliofanikiwa.
Hii ni hatua kubwa kwa wanawake wa Afrika ambayo tunaamini kuwa
itawapeleka katika hatua kubwa zaidi,”alisema Martine.
Maoni
Chapisha Maoni