Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2015

(Picha) Mwili wa Deo Filikunjombe ulivyoagwa Dar

Picha
Octoba 15,  2015 taarifa ya Majonzi ilitufikia ambapo taarifa yenyewe ilikuwa inahusu msiba wa watu wanne wakiwemo Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe na aliyekuwa Baba mzazi wa meya wa Ilala, William Silaa  baada ya kupata ajali kwenye helikopta iliyoanguka katika msitu wa mbuga ya Wanyama ya   Selous . Taarifa kuhusu Ratiba ya  kuwasili kwa miili hiyo Dar es Salaam na shughuli za kuaga miili hiyo pamoja na Ratiba ya Mazishi tayari ilitolewa, ambapo leo Octoba 17, 2015 marehemu Deo Haule Filikunjombe pamoja na wengineo waliofariki kwenye ajali hiyo ya helikopta waliagwa  Mbagala Dar es Salaam kuelekea Ludewa mkoani Njombe kwaajili ya mazishi.- Millardayo,com            

kabila la Wamakua; Kila mmakua lazima awe mchamungu

Picha
W AMAKUA   ambao jina lao pia huandikwa ( Wamakhuwa ) ni kabila kubwa lenye idadi kubwa ya watu wanaoishi hasa nchini Msumbiji upande wa Kaskazini. Lakini kwa hapa nyumbani Tanzania kuna Wamakua wanaoishi katika Mkoa wa Mtwara , Wilaya ya Masasi na Wilaya ya Nanyumbu . Kabila hili kiuhalisia lina lugha za aina mbalimbali, lakini inayotumiwa na wamakua wa hapa nyumbani ni ile ya kimakhuwa-Meetto . Wamakua Inaelezwa kuwa jamii hii ilihamia nchini Tanzania kutoka nchini Ureno na Msumbiji, kabla ya waarabu hawajaingia kwenye nchi hiyo. Wamakua ni miongoni mwa makabila ya kibantu ambao wanapatikana wilayani masasi na sehemu za Mnanje na Nanguruwe maeneo ya Newala mkoani Mtwara na Tunduru mkoani Ruvuma kusini mwa Tanzania.  Suala la dini Kila ukoo wa mmakua ni lazima uwe mcha mungu, ambapo jamii hii ilikusanyika chini ya mti ujulikanao kama Msoro na siyo mahali pengine popote. Eneo hilo lilikuwa ni eneo la mti huo, ambalo kwa kawaida lilitakiwa kuwa safi mu...

Read, Rotary wazipiga jeki shule ya msingi Msasani A&B

Picha
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Read International kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wanaojitolea katika kusaidia jamii (Rotary), wamekabidhi maktaba kwenye shule mbili za Msasani A na B jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu shuleni hapo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maktaba hizo shuleni hapo, Mkurugenzi wa Read International, Montse Pejuan, alisema lengo la maktaba hizo ni kutaka kusaidiana na Serikali ili kuinua kiwango cha elimu nchini kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu. “Kwa sasa kuna sera ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hivyo bila kushirikiana pamoja na Serikali kamwe hatuwezi kufikia malengo ya sera hiyo ndio maana tumekuwa tukijaribu kusaidia pale tunapoweza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, lengo likiwa ni katika kuhakikisha kuwa shule zote zinakuwa na maktaba nchini,” alisema Pejuan. Naye Rais wa Rotary Club of Dar Osterbay, Mohamed Versi, alisema hutoa misaada mbalimbali kwa jamii hivyo walijito...

Price Waterhouse Coopers supports Mtakuja Secondary School

Picha
 PriceWaterhouseCoopers (PWC) donated 563 books, worth TZS 4.1 million to the to the Mtakuja Secondary School (Kinondoni library).   Bachi Shirima of PriceWaterhouseCoopers handed over books to Lucy Peter, Head of the English Department.  Also present were PWC staff, library prefects and Realising Education/READ International Executive Director, Montse Pejuan. Shirika la Read International limekuwa likipambana kuhakikisha kila shule ya Msingi na Sekondari inakuwa na   Maktaba yenye vitabu kwaajili ya wanafunzi kujisomea. mpango huo umekuwa ukifanyika kwenye shule zote nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwamo makampuni ya ndani na nje ya nchi.