kabila la Wamakua; Kila mmakua lazima awe mchamungu
WAMAKUA ambao jina lao pia huandikwa (Wamakhuwa)
ni kabila kubwa lenye idadi kubwa ya watu wanaoishi hasa nchini Msumbiji upande wa Kaskazini.
Lakini kwa hapa
nyumbani Tanzania kuna Wamakua wanaoishi katika Mkoa
wa Mtwara, Wilaya
ya Masasi na Wilaya ya Nanyumbu.
Kabila hili
kiuhalisia lina lugha za aina mbalimbali, lakini inayotumiwa na wamakua wa hapa
nyumbani ni ile ya kimakhuwa-Meetto.
Wamakua
Inaelezwa kuwa jamii hii ilihamia
nchini Tanzania kutoka nchini Ureno na Msumbiji, kabla ya waarabu hawajaingia
kwenye nchi hiyo.
Wamakua ni miongoni mwa makabila ya
kibantu ambao wanapatikana wilayani masasi na sehemu za Mnanje na Nanguruwe
maeneo ya Newala mkoani Mtwara na Tunduru mkoani Ruvuma kusini mwa
Tanzania.
Suala la dini
Kila ukoo wa mmakua ni lazima uwe
mcha mungu, ambapo jamii hii ilikusanyika chini ya mti ujulikanao kama Msoro na
siyo mahali pengine popote.
Eneo hilo lilikuwa ni eneo la mti
huo, ambalo kwa kawaida lilitakiwa kuwa safi muda wote, ambalo lilitumika kuomba
amani.
Tunaelezwa kuwa kila siku asubuhi
wamakua walikuwa wakikusanyika chini ya mti huo ‘Msoro’ kwaajili ya kumuomba mungu, kwa kuwalinda
usiku mzima, huku pia wakiomba sala kwaajili ya ulinzi wa siku mpya, na baada
ya tukio hilo walielekea kwenye mihangaiko yao ya siku.
Wakati jua linapozama jamii hii
hukusanyika kwenye mti huo wa Msoro kwaajili ya kumshukuru mungu, kwa kuwalinda
kutwa nzima na kisha kumuomba tena kwaajili ya ulinzi wa usiku, tukio
linalohusisha watuwazima tu.
Hata hivyo, pamoja na mambo mengine
lakini kulikuwa na sadaka ambayo hutolewa kwaajili ya kumshukuru mungu, hasa
kabla ya msimu wa kupanda na kuvuna.
Lakini pia walimtolea sadaka mungu
hasa pale panapotokea ugonjwa, sambamba na kunapotokea kipindi cha ukame.
Pindi linapotokea tukio la ukame
watu wengi hutoa sadaka mbambali ambazo huja nazo kwenye mti wa Msoro au mti wa
mungu.
Lakini kwenye jamii hii watu ambao
hutoa sadaka huonekana watu mhimu zaidi ambao hujulikana kama ‘Mwene’ ikiwa na
maana ya (machifu), wawindaji bora na wakulima bora na maarufu au wapiganaji
wakuu.
Usikose mwendelezo...
Maoni
Chapisha Maoni