Boko Haram wauteka mji muhimu Nigeria
Wanajeshi wa serikali ya Nigeria. Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka. Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali. Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao. Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo. Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi. Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama. Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa k...