JICHO LA TEKNOLOA: Ifahamu simu mpya ya iPhone XR
Leo tunaanza kwa kuiangazia
kampuni ya utengenezaji vifaa vya kielektroniki ya Apple ambayo mwishoni mwa
mwaka jana 2018 imeingiza sokoni simu kadha wa kadha ikiwamo iPhone XR ambayo
ndiyo imepata nafasi ya kuangaziwa kwenye Jicho
la Teknolojia.
iPhone XR ni muendeleo wa
kutoa bidhaa bora kwa wateja wa bidhaa za Apple walioko kote duninia.
Kwani kampuni hiyo imekuwa na
sifa hiyo ya kutengeneza bidhaa zenye kuaminika zaidi hususan simu zake za
iPhone.
Sifa
kuu za iPhone XR
Kuna sababu nyingi za wewe
kumiliki simu hii, kwanza kabisa ni teknolojia yake ya usalama yaani Face Id
ambayo hii inakuwezesha kufungua simu yako kwa kutumia uso wako tu huku ikiwa
na kamera maalumu ya kukutambua.
Hii inamaana kwamba mtu mwingine
hawezi kufungua simu yako mbali na wewe jambo ambalo limeleta mapinduzi
makubwa.
Lakini sifa kuu nyingine ni
kwamba betri ya iPhone XR inakaa na chaji kwa saa 25 kama utakuwa ni mtu wa
kuperuzi mtandaoni basi unaweza kutumia siku nzima bila kuhitaji kuchaji tena
kwani itakuchukua saa 15.
Kama wewe unapendelea kutazama
video mbalimbali basi itakulazimu kuchaji simu yako baada ya saa 16. Na kwa
wewe unayependa kusikiliza muziki basi utasikiliza kwa muda wa saa 65 hili ni
jambo la kuvutia zaidi huku ikija na teknolojia ya fast battery charging (yaani
wireless chaging).
Hivyo kwa sifa hizo naamini
kuwa hii ni simu suluhishi kwa wote mnaopenda kuperuzi mitandaoni na kucharaza
muziki kwa muda mrefu bila kuishiwa chaji kwani hautakuwa na hofu na hili ni jambo
la kupongezwa zaidi kwa Apple kwa kuleta simu hii bora kwani nguvu ya betri hii
imeongezwa dakika 90 zaidi tofauti na matoleo yaliyopita.
Sifa nyingine ambayo hii
imekuwa ni kivutio kwa wengi ni eneo la Kamera ambayo ni ya kisasa zaidi na
inapiga picha kwa teknolojia ya hali ya juu kulinganisha na simu nyingine ikiwa
pia na uwezo wa kuchukua video hadi za 4K au HD jambo ambalo limekuwa si rahisi
kwa simu nyingin.
Simu hii inakuja ikiwa na
matoleo matatu mbayo ni GB 64, 128 na 256 ambapo ukubwa wa kila simu
unajitosheleza na hauhitaji kuongeza memory kadi.
Pia imekuja ikiwa na uwezo wa
kuonyesha rangi milioni 16, mfumo wake wa uendeshaji ni iOs 12, mtandao ni 4G
dhamana yake ni mwaka mmoja, inao uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa zaidi ya
dakika 30 bila kupata hitilafu (water proof) na kikubwa ni kuwa bidhaa zote za
Apple haziingizi virus.
Unaipataje
Wenye mamlaka ya kusambaza bidhaa zote za Apple hapa nchini ni Elite Computers ambao wanapatikana Upanga mkabala na shule ya Msingi ya Olympio, Sea Cliff Village, Viva Towers iliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Victoria Plaza (Samora) kwa Dar es Salaam na Mwanza Kenyatta Road usoni na NMB Bank au unaweza kuwasiliana nao kwa namba O786 176 700.
Wapo pia kwenye mitandao ya kijamii ambapo Facebook ni Elite Computers na Instagram ni Elite Computers Tanzania. Elite Computers mbali na simu pia wanabidhaa kama i Mac, Apple Tv, MacBook Pro, iPad, iPod maalumu kwa ajili ya muziki pia wanatoa huduma ya matengenezo kwa bidhaa zote.
Kosa simu zoote 2019 lakini siyo iPhone XR, kwani nisimu inayoendana na mazingira halisi ya kitanzania hususan suala zima la Chaji, hivyo watafute Elite Computers ili ukamate ya kwako sasa kwa mawasiliano hayo hapo juu.
Maoni
Chapisha Maoni