Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2019

JICHO LA TEKNOLOA: Ifahamu simu mpya ya iPhone XR

Leo tunaanza kwa kuiangazia kampuni ya utengenezaji vifaa vya kielektroniki ya Apple ambayo mwishoni mwa mwaka jana 2018 imeingiza sokoni simu kadha wa kadha ikiwamo iPhone XR ambayo ndiyo imepata nafasi ya kuangaziwa kwenye Jicho la Teknolojia.   iPhone XR ni muendeleo wa kutoa bidhaa bora kwa wateja wa bidhaa za Apple walioko kote duninia. Kwani kampuni hiyo imekuwa na sifa hiyo ya kutengeneza bidhaa zenye kuaminika zaidi hususan simu zake za iPhone. Sifa kuu za iPhone XR Kuna sababu nyingi za wewe kumiliki simu hii, kwanza kabisa ni teknolojia yake ya usalama yaani Face Id ambayo hii inakuwezesha kufungua simu yako kwa kutumia uso wako tu huku ikiwa na kamera maalumu ya kukutambua. Hii inamaana kwamba mtu mwingine hawezi kufungua simu yako mbali na wewe jambo ambalo limeleta mapinduzi makubwa. Lakini sifa kuu nyingine ni kwamba betri ya iPhone XR inakaa na chaji kwa saa 25 kama utakuwa ni mtu wa kuperuzi mtandaoni basi unaweza kutumia siku nzima bila kuhitaji ...