NEC yatoa maamuzi kuhusu rufaa ya uchaguzi mdogo
Mgombea udiwani wa chama cha Wananchi (CUF), Mdohoma Bashiru Ismaili amerejeshwa kwa mara nyingine katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya udiwani, wa kata ya Kibutuka katika halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi, baada ya rufaa yake kutolewa maamuzi bila ya kupingwa. Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hamis Mkunga leo Septemba 30, 2018 na kusema kuwa maamuzi hayo yamefanyika kwa kufuatia kikao kilichoketi leo na kukubaliana na maelezo yaliyotolewa na mkataji rufaa huyo ambaye alitaka kurejeshwa kuwa mgombea udiwani katika Kata ya Kibutuka kupitia chama hicho. "Tume katika kikao chake cha tarehe 30 Septemba 2018, imekubaliana na maelezo ya mrufani na kuelekeza arejeshwe kuendelea kuwa mgombea Udiwani katika Kata ya Kibutuka, Halmashauri ya wilaya ya Liwale kwa kuwa imejiridhisha kwamba mrufani wakati wa kujaza fomu yake ya uteuzi Na. 8C alianza na jina la mwisho likifuatiwa na majina mengine kwa...