Okwi akabidhiwa kwa bilionea Afrika
STRAIKA wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi, ananukia utajiri katika klabu
hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba uongozi wa klabu hiyo unataka
kumkabidhi kwa mdhamini mpya wa timu hiyo ambaye ni mmoja wa matajiri
vijana barani Afrika, Mohamed Dewji, kwa ajili ya kulipiwa kila kitu.
Okwi
aliiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa
jadi, Yanga, katika mchezo uliochezwa Machi 8 mwaka huu na pia dhidi ya
Mtibwa Sugar mwishoni mwa wiki iliyopita, huku straika huyo akifunga
mabao hayo katika mazingira magumu, mabao yanayotajwa kuwa ni moja ya
mabao mazuri msimu huu.
Mbali na mabao hayo, Okwi pia amekuwa msaada mkubwa pale Simba wanapocheza, kwani kama hatafunga mwenyewe atatoa pasi ya mwisho, kitu ambacho kinampa heshima kubwa ambapo anatarajiwa tena leo kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Mgambo JKT, katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Taarifa za
uhakika ambazo DIMBA Jumatano imezinasa zinadai kuwa viongozi wa klabu
hiyo wanafikiria kumkabidhi kwa Mohamed Dewji (MO), anayetajwa kurudisha
udhamini wake kwa klabu hiyo, ambayo kwa sasa ipo nafasi ya tatu katika
msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
DIMBA Jumatano limeelezwa kuwa Okwi atakuwa akipata huduma zote atakazozihitaji, ikiwamo mshahara na marupurupu mengine, ili kuzidi kumtia moyo kuendelea kuifanyia Simba makubwa.-Dimba
Mbali na mabao hayo, Okwi pia amekuwa msaada mkubwa pale Simba wanapocheza, kwani kama hatafunga mwenyewe atatoa pasi ya mwisho, kitu ambacho kinampa heshima kubwa ambapo anatarajiwa tena leo kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Mgambo JKT, katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
DIMBA Jumatano limeelezwa kuwa Okwi atakuwa akipata huduma zote atakazozihitaji, ikiwamo mshahara na marupurupu mengine, ili kuzidi kumtia moyo kuendelea kuifanyia Simba makubwa.-Dimba
Maoni
Chapisha Maoni