Ngassa ashtakiwa Zimbabwe

STRAIKA wa Yanga, Mrisho Khaflan Ngassa ambaye Jumapili iliyopita alipeleka kilio kwa timu ya Platinum ya Zimbabwe kwa kupachika mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-1 ambao timu yake iliupata, ameshtakiwa katika ripoti iliyotolewa na kocha mkuu wa timu hiyo, Norman Mapeza.
Ngassa aliyeonyesha kiwango katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, ametajwa kama ndiye aliyechagiza ushindi huo, pia alikuwa ni kikwazo kwa timu hiyo.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4w1GYKtqyCzn-cK20D78IV66Cq6gtmmw074t-D517eQ2vKQu_WuMAAoy0SBdvc0m-aCKgiEZC4o9uhS5SlcmyTCy00M1VU42a5uDOUHshNluQW7EdVaJlPFiAd-_8gY3y0BY94HEf9h0-/s1600/NGASSA+SHANGWE+ZA+BAO.jpg
Mapeza alitoa ripoti hiyo na kubainisha mapungufu na changamoto zilizoifanya timu yake kupoteza mchezo huo muhimu wa ugenini.
"Ngassa ndiye kikwazo hasa alimsoma mlinzi wetu, Kelvin Moyo na alikuwa akipita sana kwake ni mchezaji hatari sana," ilisema sehemu ya ripoti hiyo iliyonukuliwa na mtandao wa New Zimbabwe.
Pia kocha huyo ameeleza pengo jingine lililoiathiri timu yake ni kukosekana kwa mshambuliaji wao mkongwe, Donald Ngoma, aliyeondoka siku mbili kabla ya mechi hiyo.
Mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakilaumu benchi la ufundi huku wakieleza wasiwasi wao wa kuweza kuifunga Yanga kwa idadi kubwa ya mabao kama hiyo.
Katika hatua nyingine, lawama zaidi zimeelelekezwa katika safu ya ulinzi ambayo iliruhusu mabao ya mapema na pia kushindwa kuikabili kasi ya washambuliaji wa Yanga na hivyo kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara.
Timu hizo zitacheza mechi ya marudiano Aprili 4, mchezo utakapigwa nchini Zimbabwe, ambapo Yanga inapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutokana na kuwa na mtaji wa ushindi wa mabao 5-1.-Dimba

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4