Mbunge ashauri uchaguzi Serikali za mitaa
MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ally
Keisy Mohamed (CCM), ameitaka Serikali kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa sehemu zote itakapothibitika kwamba wahamiaji walishiriki kupiga kura.
Ally Keisy |
Akiuliza swali bungeni jana, Keisy
alisema maeneo mengi ya mipakani wahamiaji walipiga kura katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
“Kwa nini Serikali isiamuru sasa
uchaguzi urudiwe katika maeneo yote ambayo wakimbizi walishiriki kupiga kura
kwa kuwa wakimbizi hawa kwa kiasi kikubwa wanalindwa na maofisa uhamiaji?”
alihoji Keisy.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey
Mwanri alisema katika uchaguzi huo majina ya wagombea yalikuwa yanatangazwa
mapema kutoa fursa kwa watu kuweka pingamizi.
“Vilevile majina ya wapiga kura
yalikuwa yanabandikwa mapema hali inayowezesha mtu yeyote kupeleka pingamizi
lake kupinga majina hayo,” alisema.
Awali akijibu swali la msingi la
Mbunge wa Viti Maalum, Josephine Genzabuke(CCM), Mwanri alisema endapo
wapo wakimbizi waliothibitika kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
kwa Mkoa wa Kigoma, Serikali ipo tayari kufanya uchunguzi juu ya madai haypo.
Hata
hivyo ni jukumu la viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa na wananchi kuwabaini watu ambao siyo raia au
wakazi wa eneo husika na kutoa taarifa kwa mamlaka husika hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa
sheria,” alisema.Katika swali lake, Genzabuke alitaka kauli ya Serikali kuhusu wakimbizi waliopiga kura katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kigoma.
Maoni
Chapisha Maoni