Mama ajifungia chumbani, ajichoma moto na mwanae

ANGELINA John (22) mkazi wa Kijiji cha Mbulu wilayani Kahama, amefariki baada ya kujifungia chumbani na mtoto wake kabla ya kujimwagia mafuta na kujichoma moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamungisha   alisema tukio hilo lilitokea  juzi mchana     baada ya Angelina kujifungia na mwanae   John (2) na kujimwagia mafuta ya taa na kujichoma moto.http://ewallpaperhub.com/wp-content/uploads/2015/01/Website-Fire-Backgrounds-pics.jpg

Kwa mujibu wa kaka wa Angelina aliyejitambuklisha kwa jina la Kanuti John, ilielezwa kuwa baada ya kujifungia ndani na mwanae alilimwagia mafuta godoro, nguo  na vyombo vya plastiki  kwa lengo la kujiua kutokana na kuwa na mgogoro na mzazi mwenzake.

Kanuti alieleza kuwa baada ya kupata taarifa za kuwapo   moto katika nyumba anayoishi dada yake,alikwenda huko mbio na kukuta moshi mkubwa ukifuka kutoka ndani ya chumba chake.



Alivuja mlango wa chumba hicho,  akaingia kuingia ndani  kujaribu kumuokoa dada yake lakini alikuta akiwa kitandani na mtoto wake wakiwa tayari wamekwisha kufariki dunia.



“Inaonekana alijifungia ndani na kujilipua kwa moto baada ya kujimwagia mafuta…ndani tulikuta harufu kali ya mafuta ya taa, mtoto wake tulimkuta akiwa katika harakati za kujaribu kujiokoa,” alisema kaka wa marehemu.-mtanzania

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4