Goran: Nina saa tisa tu Simba kubeba ubingwa

KOCHA Mkuu wa Simba Mserbia, Goran Kopunovic, amekiangalia kikosi chake na kusema amebakisha saa tisa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

http://galacha.com/kandanda_admin/uploads/posts/636841b50e7d4d876862ec7a83150701.jpg
Kocha Goran
Simba iliyosaliwa na mechi sita kila moja ikiwa inachezwa kwa dakika 90 hivyo kufanya jumla ya dakika 540 ndani ya mechi hizo.

Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 32, ikitanguliwa na Azam FC yenye pointi 37 na Yanga (38) waliopo kileleni.

Akizungumza na BINGWA juzi, Kopunovic alisema baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa anaangalia ubingwa ndani ya dakika hizo.

Kopunovic alisema pamoja na Yanga na Azam FC kujihakikishia ubingwa, lakini ataendelea na mipango yake ya kuiwezesha Simba kushinda mechi zilizosalia.
“Katika dakika hizi zilizosalia naweza kufanya jambo kubwa sana na kubadilisha msimamo wote wa ligi, angalia sisi tupo nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi tano na vinara,” alisema Kopunovic.

Alisema tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo imekuwa ikishinda na kufungwa, ingawa anaamini ubingwa unaweza kupatikana kwa timu nyingine ikifanya vibaya na wao kushinda.

Simba imesalia kucheza na Mbeya City mchezo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, Mgambo Shooting, Ndanda FC, Azam FC na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Kagera Sugar, Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4