Australia yafanya mabadiliko kwenye chumba cha Marubani
Waziri mkuu msaidizi wa Australia Warren
Truss ametangaza kuwa kuanzia sasa hakuna Rubani kubaki mwenye kwenye chumba cha Marubani, hii ikiwa ni baada ya ajali ya ndege ya Ujerumani
kuangushwa kwa makusudi na Rubani msaidizi huko Ufaransa na kuua watu
wote ndani yake ambao walikua wanazidi 150.
Truss amesema mashirika ya ndege ya
Australia ikiwemo Qantas na Virgin Australia wameanza kuyafanyia kazi
mabadiliko ya usalama ambapo kama wako wawili na mmoja akawa
anataka kutoka labda kwenda Toilet, inabidi muhudumu mmoja wa ndege
aingie kwenye chumba hicho ndio rubani mmoja atoke.
Waziri
mkuu msaidizi wa Australia Warren Truss ndio kaitangaza hii, na ni
baada ya ajali ya ndege ya Ujerumani kuangushwa kwa makusudi na Rubani
msaidizi huko Ufaransa na kuua watu wote ndani yake ambao walikua
wanazidi 150.
Truss amesema mashirika ya ndege ya
Australia ikiwemo Qantas na Virgin Australia wameanza kuyafanyia kazi
mabadiliko ya usalama ambapo kuanzia sasa hakuna cha Rubani kubaki
mwenyewe kwenye chumba cha Marubani, kama wako wawili na mmoja akawa
anataka kutoka labda kwenda Toilet, inabidi muhudumu mmoja wa ndege
aingie kwenye chumba hicho ndio rubani mmoja atoke.
Mabadiliko haya yameanza kufanyiwa kazi
toka Jumatatu mchana March 30 2015 ambapo mwanzoni ilikua inaruhusiwa
kwa Rubani mmoja kupaki kwenye chumba cha kurushia ndege.
Hii yote imekuja baada ya Rubani msaidizi
kwenye ndege ya Ujerumani iliyoanguka Ufaransa kugundulika kwamba
aliiangusha ndege kwa makusudi na ni baada ya Rubani mkuu kutoka nje ya
chumba cha Marubani, alipotaka kurudi akakuta mlango umefungwa, yaani
rubani msaidizi ndio kajifungia na akaiangusha ndege kwa makusudi.-Millardayo.com
Maoni
Chapisha Maoni