Afrika inaongoza kwa magonjwa
ASILIMIA
25 ya magonjwa wanaougua binadamu hapa duniani yanapatikana katika bara la
Afrika.
Hayo
yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.
Seif Suleiman Rashid katika mkutano wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji (TSA).
Dk.
Seif Suleiman Rashid amesema kuwa kutokana na wingi wa maradhi kuliandama bara
hilo imekuwa sababu kubwa ya kuwepo kwa hitaji la madaktari zaidi.
DK.
Rashid amesema kuwa pamoja na Afrika kukumbwa na maradhi zaidi lakini hadi sasa
ina asilimia tatu ya madaktari bingwa hususan katika fani ya upasuaji ambao
hawakidhi mahitaji halisi ya kutoa huduma hiyo.
‘Bado
tuna safari ndefu sana ya kukabiliana na upungufu huu wa madaktari bingwa katika
fani ya upasuaji ambayo ni muhimu katika maisha yetu,”.
Waziri
amekimwagia sifa Chama cha Madaktari bingwa wa upasuaji (TSA) kwa juhudi
wanazozifanya kupambana na tatizo la upungufu wa madaktari bingwa.
Amesema
kuwa ili kuhakikisha kunapatikana ongezeko la madaktari bingwa, serikali imekuwa
karibu na chuo cha madaktari bingwa kilichopo Arusha kinachotoa elimu ya juu
katika fani ya upasuaji kwa kuwapa misaada ya hali na mali.
Akizungumzia
changamoto zinazolikabili bara la Afrika katika fani ya utabibu amesema ni
pamoja na kutokuwepo kwa miundo mbinu, vitendea kazi pamoja na rasilimali watu.
“Tunahitaji
kuwekeza nguvu nyingi kuweza kufikia malengo ya milenia kama kweli tunahitaji
kufanikiwa katika hili lazima tuweke nguvu ya pamoja kati ya Wananchi na serikali,”.
Katika
mkutano huo Dk. Rashid alitoa vyeti kwa madaktari bingwa wa upasuaji 61 toka
katika chuo cha kitabibu kilichopo Arusha pamoja na vyeti kwa madaktari bingwa
wastaafu katika fani ya upasuaji ambao ni Profesa Philemon Sarungi, Profesa
Joseph Shija na Profesa Cray Bernard.
Kwa
upande wake Rais wa TSA, Paul Marealle amesema kuwa sekta ya afya hapa nchini
bado inahitaji nguvu ya ziada kuiweka sawa.
Amesema
kuwa vifo vingi vya akina mama na watoto hususani katika maeneo mengi hapa
nchini ni matokeo ya nchi kushindwa kuwekeza inavyotakiwa katika sekta hiyo.
Maoni
Chapisha Maoni