Njia tano za kuongeza mauzo kwenye biashara yako
KILA mjasiriamali anafahamu kuwa fedha ndio damu ya biashara.
Kama hakutakuwa na mzunguko wa fedha wa kutosha kwenye biashara ni sawa na mtu
ambaye hana damu ya kutosha na hivyo itasababisha kufa kwa biashara.
Njia kubwa
ya kuongeza mzunguko wa fedha kwenye biashara yoyote ni kuongeza mauzo. Hii ina
maana kwamba tayari unayo huduma au biadhaa inayohitajika na kwa bei unayouzia
unapata faida, hivyo utakapouza mara nyingi zaidi utapata faida kubwa zaidi.
Leo tutajadili njia tano unazoweza kutumia kuongeza mauzo kwenye
biashara yako. Kupitia njia hizi utaweza kuuza zaidi kwa wateja ulionao sasa,
kuuza kwa wateja wapya na hata kuwafanya wateja wako waendelee kuwa na wewe.
Jenga uhusiano
mzuri na wateja wako
Njia ya kwanza ni kujenga uhusiano mzuri na wateja wako.
Biashara za zama hizi zinajengwa kwa uhusiano. Mteja atakuwa tayari kununua
bidhaa au huduma kwa mtu ambaye anaona anamjali na anajali mahitaji yake. Kwa
mfano; kama wewe ungekuwa unataka kununua kitu na kuna wauzaji wawili, mmoja ni
rafiki yako na mwingine ni mtu ambaye humjui kabisa, utanunua wapi? Moja kwa
moja utanunua kwa rafiki yako kwa sababu unajua hawezi kukuuzia kitu kibaya au
kukulaghai. Omba namba zao za simu za wateja wako na mara kwa mara wasiliana
nao kuwajulia hali na kujua bidhaa au huduma uliyowauzia inawasaidiaje.
Onesha moyo wa
kuwasiadia
Ili kuweza kupata wateja wengi na kuongeza mauzo zaidi lengo
kubwa la biashara yako inabidi iwe kuwasaidia watu. Bidhaa au huduma unayotoa
inabidi iwe inawasaidia watu kutatua matatizo au changamoto wanazokutana nazo.
Kwa mantiki hii unapofanya biashara na wateja wako hakikisha unawaeleza vizuri
matumizi ya bidhaa au huduma yako na faida zake kwao. Wapatie maelezo ambayo
una uhakika yatawasaidia, badala tu ya kuwauzaia na kuwaacha wakafikirie
wenyewe ni jinsi gani itawasaidia.
Jenga tabia ya
kuwapa ofa wateja
Tabia moja ya binadamu ni kwamba hatupendi kupitwa na kitu. Ila
pia tunapoona kitu kinapatikana wakati wowote ambao tunakitaka, shauku ya
kukipata hupungua. Kwa mfano kama mteja anajua kwamba wakati wowote anaweza
kupata bidhaa au huduma unayotoa anaweza asiwe na shauku kubwa. Ila kama ukitoa
ofa ambayo inaisha baada ya muda mfupi wateja wako watachuku hatua ya kufanya
manunuzi haraka ili wasipitwe na ofa hiyo. Hivyo toa ofa za mara kwa mara kwa
wateja wako na hii itakusaidia kuongeza mauzo.
Omba wateja
zaidi kutoka kwa wateja wako
Wateja wako wana ndugu, jamaa na marafiki ambao nao wanaweza
kuwa wateja wako. Watumie wateja hawa kupata wateja wengi zaidi. Kwa kuwa
wateja wako wameshakuamini waombe wawaambie jamaa zao kuhusu biashara yako.
Wakati mwingine waombe mawasiliano ya jamaa zao hao na kisha wasiliana nao
ukiwaambia kwamba jamaa yao ambaye ni mteja wako ameona wanaweza kufaidika na
bidhaa au huduma unayotoa. Njia hii itakuongezea wateja zaidi.
Waridhishe
Pamoja na yote hayo ambayo tumejadili hapa cha muhimu kabisa ni
kuwaridhisha wateja wako. Hakikisha mteja wako anaridhika kwa bidhaa au huduma
uliyompatia kwa gharama alizolipia. Kwa njia hii wateja wako wataendelea kuwa
na wewe kwenye biashara na watakuletea wateja wengi zaidi. Kumbuka mteja bora
wa kesho kwenye biashara yako ni mteja uliyenaye leo, hivyo hakikisha
unaendelea kumtunza ili uendelee kufanya nae bishara.
Ongeza mauzo zaidi ya biashara yako kwa kuongeza wateja zaidi,
kuuza zaidi kwa wateja ulionao sasa na kuwatunza wateja ulionao sasa ili
kuendelea kufanya nao biashara zaidi.
Ni kweli kabisa Ila mm Natalia hatua za utambulisho WA bidaa
JibuFuta