Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki akubali kuachia madaraka

Awali, Al-Maliki alipinga uteuzi huo na kusisitiza kuwa hangekabidhi madaraka kwa kuwa ilikuwa kinyume na sheria, hatua iliyosababisha kukosolewa ndani ya nchi na kimataifa. Wanasiasa hao wote wanatoka chama cha kishia cha Dawa, ambacho ndicho kilichopata viti zaidi katika uchaguzi wa wabunge uliyofanyika mwezi April.
Marekani imekaribisha uamuzi Maliki na mshauri wa masuala ya usalama wa rais Barack Obama Suzan Rice, ameuelezea kama hatua muhimu kuelekea kuiunganisha tena nchi hiyo.
Mgogoro wa madaraka nchini Iraq unaelezwa kuwa sababu ya kuimarika kwa kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola ya Kiislamu IS, ambalo limeyateka maeneo kadhaa ya nchi hiyo katika juhudi za kuunda taifa linaloendeshwa chini ya misingi ya sheria za Kiislamu.
Maoni
Chapisha Maoni