Yanga yapata ulaini Tunisia
YANGA imepata mteremko kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Etoile ya Tunisia, kwani imepata mbinu zitakazowawezesha kuwashika pabaya wapinzani wao hao. Mchezo huo ni wa raundi ya pili ya michuano hiyo ambapo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Matokeo hayo yanaipa kibarua kigumu Yanga mjini Tunis kwani watalazimika kushinda au kupata sare ya zaidi ya mabao 2-2 ili iweze kusonga mbele na kutinga hatua ya mtoano kuwania tiketi ya makundi. Kwa kufahamu ugumu wa mchezo wa marudiano, Yanga imepanga kufanya kila mbinu wanazoweza ili kuwajengea mazingira mazuri ya kushinda na kuwatoa Etoile. Miongoni mwa mbinu hizo ni kuwahi mapema nchini Tunisia ili kuzoea hali ya hewa ya huko ambayo ni ya baridi na kukutana na Watanzania waishio huko ili waweze kuwapa mikakati ambayo wanaweza kuitumia kukwepa hila za wapinzani wao hao na kushinda. ...