Machapisho

Okwi: akili kubebwa J’mosi

Picha
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi, amemshukuru mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Jumamosi iliyopita, Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, kwa kuongeza dakika tano baada ya dakika 90 za muda wa kawaida, hivyo kuwawezesha kufunga bao pekee lililoipa timu yake ushindi wa 1-0. Okwi alifunga bao hilo dakika ya tatu kati ya tano za muda wa nyongeza, wakati timu hizo zikiwa hazijafungana katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mganda huyo alifunga bao hilo kwa staili ya aina yake, akipiga shuti kali akiwa umbali wa mita 25 kutoka lango la Mtibwa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Abdi Banda. Kabla ya kufunga bao hilo wakati baadhi ya mashabiki wakiwa wametoka uwanjani wakijua matokeo ni suluhu, aliwahadaa mabeki na kumchungulia kipa wa wapinzani wao hao alivyokaa na kupiga mpira mrefu uliokwenda moja kwa moja wavuni. Okwi alisema miongoni mwa watu anaowashukuru kwa kumpa nguvu ya kutafuta bao ni mwamuzi huyo, b...

Kocha Platinum ajuta kuifahamu Yanga

Picha
KOCHA wa Platinum ya Zimbabwe, Norman Mapeza, amesema hatakisahau kikosi cha Yanga kutokana na kuwafanyia mauaji katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Norman Mapeza Katika mchezo huo uliokuwa na msisimko wa aina yake, Yanga ilishinda mabao 5-1, wafungaji wakiwa ni Salum Telela, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe na Mrisho Ngassa, aliyecheka na nyavu mara mbili. “Nimekuja Tanzania nikitambua nakuja kucheza na timu imara, nikawasisitiza wachezaji wangu kuwa makini kuepuka kufungwa mabao mengi, lakini wameshindwa na kujikuta tukifungwa mabao mengi.” Alisema kuwa kikosi kizima cha Yanga kinatisha, hivyo hawezi kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja, zaidi ya kuona wanakwenda kujipanga vipi kwao waweze kulipiza kisasi. Aliionya Yanga kutobweteka na ushindi wao huo na kujiona wamefanikiwa kuwatoa, kwani iwapo wao wameweza kupata mabao matano wakiwa nyumbani kwao, nao hawashindw...

Goran: Wembe ni ule ule Tanga

Picha
BAADA ya kuibuka na ushindi mara tatu mfululizo, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, amesema wembe ni uleule katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Maafande wa Mgambo JKT. Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao, Simba, tayari kimeshawasili jijini Tanga kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kesho Uwanja wa Mkwakwani. Akizungumzia mchezo huo, Goran alisema amefanya maandalizi mazuri katika kikosi chake, huku akiwapa majukumu wachezaji wake kuhakikisha wanarudi jijini Dar es Salaam wakiwa na pointi tatu mkononi. Alisema ametumia siku mbili kwa ajili ya kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, hivyo tayari kikosi chake kipo imara kuwavaa Mgambo. “Kila mtu anafahamu jukumu lake, tumepata ushindi katika mchezo dhidi ya Mtibwa, hivyo pia tunakwenda kwa wapinzani wetu tukiwa na akili ya kutaka kupata ushindi,” alisema. Goran alisema anatambua anakutana na timu ngumu na kutumia vyema uwanja wa nyumbani, lakini kwa upande wake atahakikisha vijan...

Ngassa alamba dume TP Mazembe

Picha
MABAO sita aliyofunga msimu uliopita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na matatu ya Kombe la Shirikisho msimu huu, yamemsafishia njia Mrisho Ngassa kutua TP Mazembe ya DRC, ikiwa ni kutokana na mpango unaosukwa na Mtanzania Mbwana Samatta, anayeichezea timu hiyo. Msimu uliopita, Ngassa aliifungia Yanga mabao hayo ndani ya mechi nne za hatua ya awali na ya kwanza na kumfanya kuwa miongoni mwa wafungaji bora wa michuano hiyo. Kutokana na mafanikio hayo, mawakala wa klabu mbalimbali barani Afrika na kwingineko, walianza kufuatilia nyendo za straika huyo kuona kama ana kiwango cha kumwezesha kuzichezea timu zao. Na kwa kuwa Samatta naye anatoka Tanzania, waliamua kumtumia kujua ubora wa winga huyo machachari. Kutokana na hilo, Samatta alimtumia ujumbe Ngassa kumtaka kudhihirisha ubora wake wa kucheka na nyavu msimu huu wakiwa wanashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, jambo ambalo mkali huyo amelifanya ndani ya mechi tatu za kwanza kwa kufunga mabao matatu. ...

Papa Francis atoa ishara za kujiuzulu

Picha
Papa Francis na alyiekuwa papa Benedict Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu. Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya pili tangu achaguliwe,Papa Francis amesema kuwa anahisi kwamba uongozi wake katika kanisa hilo hautaendelea kwa kipindi kirefu. Amesema kuwa hatua ya Benedict kujiuzulu mwaka 2013 ni ya ujasiri na haifai kuchukuliwa kama ya kipekee. Papa Benedict ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tangu papa Gregory wa 12 mwaka 1415. Papa Francis anasema kuwa anatamani maisha yake ya kuwa muhubiri na angependelea kuzuru maeneo kadhaa bila kujulikana.-BBC

Mamia ya watoto watekwa Sudan Kusini

Picha
Umoja wa Mataifa umesema kuna uwezekano mkubwa kwamba watoto wa kiume waliotekwa hivi karibuni huko Sudan Kusini walichukuliwa na kundi lililo upande wa serikali. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto, UNICEF, limesema idadi ya watoto waliochukuliwa na wapiganaji wa Shilluk wa Johnson Oloni walikuwa mamia, na sio themanini na tisa kama ilivyodhaniwa hapo awali. Watoto wa kiume wa Sudan Kusini Mhariri wa BBC wa masuala ya Afrika, Mary Harper anasema kwa zaidi ya mwaka mmoja, jeshi la Sudan Kusini na wapiganaji wanaowaunga mkono wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi yanayomtii aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar. Bwana Oloni pia ana cheo cha meja jenerali katika jeshi la Sudan Kusini. Afisa wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, Claire McKeever ameiambia BBC kwamba shirika hilo limekuwa likijaribu kuiomba serikali kuwatafuta wavulana lakini muda unazidi kuyoyoma: "Jibu tulilopata wakati fulani ni kw...

MZEE YUSUPH: Naona fahari kuwa na wake wengi

Picha
Unafahamu kama Mzee Yusuph anasikia raha kuwa na wake wengi, huku akihakikisha anawatimizia wote mahitaji yao? Fuatana nami ufahamu mengi zaidi kuhusiana na suala la ndoa kwa nguli huyo wa muziki wa taarabu hasa wenye vionjo vya mahaba. Swali: Katika maisha yako umeoa mara ngapi? Mzee Yusuph: Nimeoa mara tano, nilioa mke wa kwanza tukashindwana nikamuacha, wa pili nikamuacha, wa tatu pia nilimuacha lakini wa nne na wa tano nipo nao. Swali: Kuna sababu kubwa ambayo unaamini mwanamke akiifanya, huwezi kuvumilia zaidi ya kumuacha? Mzee Yusuph: Sina kosa maalumu, inapotokea mwanamke anakuwa mjuba nafahamu ameshachoka ninamuacha aende zake, lakini kukwambia kuwa hili ni kosa maalumu mwanamke akifanya namuacha sina. Swali: Mke wa kwanza ulioa ukiwa na umri gani? Mzee Yusuf: Nao...