Machapisho

Tanzania, Ufaransa waanzisha kundi la kirafiki

Picha
UBALOZI wa Ufaransa nchini umeanzisha kundi la kirafiki kati ya Tanzania na Ufaransa, kwa ajili ya kubadilishana uelewa katika masuala mbalimbali ikiwemo siasa, sayansi, utamaduni na uchumi. Balozi wa Ufaransa nchini, Bertha Semu-Somi, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mjini Dar es Salaam. Alisema kikundi hicho kitazinduliwa rasmi Februari 20, mwaka huu nyumbani kwa balozi na kwa kuanzia kitakuwa na wajumbe 50 ambapo baadaye wataendelea kuongezeka. “Wajumbe wa kikundi watakuwa wanakutana mara tatu kwa mwaka kwa ajili ya kubadilishana mawazo na ujuzi, ajenda mbalimbali zitajadiliwa zikiwemo za kisiasa, elimu na uchumi. Alisema wapo Wafaransa wanaohitaji kuijua zaidi Tanzania na wapo Watanzania wanaohitaji kujua utamaduni wa Wafaransa, hivyo kupitia kikundi hicho kila upande utanufaika. “Lengo ni kuunganisha watu tofauti tofauti, kundi litakuwa uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume wa Kitanzania na Ufaransa kwa ajili ya ma...

Tanesco haiwezi kuwalipa wateja waliopata majanga ya moto – Serikali

Picha
Serikali imesema Shirika la Umeme nchini (Tanesco) haliwezi kuwalipa fidia wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme, kwani ni kuliongezea mzigo.   Hayo yalisema na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, wakati akizungumza na NIPASHE juu ya kuwapo kwa sheria ya fidia kwa wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima.   Silima alisema suala la Tanesco kulipa fidia kwa wananchi waliopatwa na majanga ya moto yaliyosababishwa na hitilafu ya umeme ni jambo gumu ambalo haliwezi kutekelezwa kwa haraka.   Alisema Tanesco ina majukumu mengi ikiwamo la kuhakikisha wananchi wanapatiwa umeme, hivyo kuliongezea mzigo mwingine ni kutaka kulifilisi.   Aliongeza kuwa mbali na kutokea kwa majanga ya moto mara kwa mara yanayosababishwa na hitilafu ya umeme, siyo kweli kwamba Tanesco limehusika moja kwa moja kusabab...

Wezi wa kompyuta wameiba dola bilioni 1

Picha
Genge la wezi wa kompyuta limefanikiwa kuiba takriban dola bilioni moja kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30. Kampuni inayosimamia usalama wa programu ya kompyuta inayohakikisha data ya wateja iko salama Kaspersky Lab imesema katika ripoti yake maalum. Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya ya wezi wa Kompyuta wanaotumia mbinu mpya ya kudakua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kupora pesa . Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao . Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza. Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo. Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol . Kwa mu...

Sitta amsimamisha kazi bosi wa bandari

Picha
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - Nimemsimamisha kazi kwa Muda Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Ndgu.Madeni Kipande leo hii trh 16 Februari 2015 ili kupisha uchunguzi unaohusu tuhuma mbalimbali zinazomkabili. Tuhuma hizo ni Pamoja na manung'uniko kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi .Hali hii inatokana na kutotabirika kwa taratibu na kukosekana kwa uwazi , pamoja na taratibu hizo kuingiliwa na mamlaka. Aidha tuhuma nyingine ni mahusiano yasiyoridhisha kati ya Uongozi wa Mamlaka ya Bandari na wadau wake muhimu na Mahusiano mabaya sehemu ya kazi. Kufuatia hali hii,nimeteua Tume ya kuchunguza suala hili na nimeipa muda wa wiki mbili Kukamilisha kazi hii na kunipatia taarifa. Majina ya Tume hiyo ni Kama ifuatayo :- 1.Jaji Mstaafu Agusta Buheshi-Mwenyekiti. 2.Ndgu.Ramadhan Mlingwa-Mjumbe 3.Eng.Samson Luhigo-Mjumbe 4.Ndgu.Happiness Senkoro-Mjumbe 5.Ndgu.Flavia...

Taarifa nyingine ya aliyejinyonga baada ya matokeo kutangazwa

Picha
Imekuwa kawaida kila mwaka pale ambapo matokeo yanapotoka watu wengenge utalajia mambo mazuri ata yulealiye kuwa kilaza dalasani naye anaamini atafaulu tu ila matokeo yake mambo yanakuja kutokana na kile ulicho panda kama ulipanda mawe basin ni mawe unatakiwa kuvuna Kinachosikitisha Zaidi ni pale wanapo chukua hatua kama huyu Kijana mmoja ajulikanaye kwa jina John Maduhu wa Kijiji cha Pandagichiza, Wilaya ya Shinyanga vijijini kaamua kujinyonga baada ya matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka jana kumjia vibaya, akiongea na mwandishi, kaka wa marehemu alisema kuwa baada ya matokeo kutoka, JOhn   alitoweka nyumbani                                     

Amkodishia mkewe mume wa 'kumhudumia'

Picha
Mtu mmoja katika mahakama ya Kwale nchini Kenya ameshtakiwa kwa kumkata pua na mkono mkewe ambaye anamshuku kwa kufanya uasherati. Kulingana na gazeti la the Nairobian nchini Kenya,Chirope Mwaruwa anadaiwa kumkodisha mwanamume ili kulala na mkewe mjamzito akidai kwamba ana matatizo. Alishtakiwa kwa kumshambulia mkewe Sada Dzea katika kijiji cha Mukundi taarafa ya Mangawani ,kaunti ya Kwale. Kulingana na upande wa mashtaka Dzea mara ya kwanza alimkataa mtu aliyekodishwa na mumewe wafanye naye tendo la ngono akiwa mjamzito. Baada ya Dzea kukataa mumuwe alianza kumshtumu kwa kufanya uzinzi huku akitaka kumvua nguo kwa lengo la kutafuta ushahidi. Na alipokasirishwa na shtuma hizo Dzea alidaiwa kumtembelea mtu huyo aliyekodishwa na mumewe ili afanye naye tendo la ngono kwa lengo la kumfurahisha mumewe. lakini kabla ya yeye kufika kwa mawanmume huyo mumewe mwenye wivu mwingi alidaiwa kumvamia na kuanza kumshambulia-bbc

Kauli nyingine mpya ya LadyJay Dee kuhusiana na ndoa yake

Picha
  Baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali ambazo zinaelezea mgogoro wa wanandoa kati ya Lady JayDee na aliyekuwa mmewe Gadna.kunataarifa mpya iliyotolewa na mwanadada Jaydee ambaye amefunguka ya moyoni kuhusu kuvunjika kwa ndoa hiyo     "Hatuja achana niliamua kumuacha.Nimemuacha kutokana na kuwa Ndoa inatakiwa iwe na maelewano,furaha,amani na upendo.ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo,sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuiridhisha jamii.sioni kujishushia heshima,ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asie na heshima,anae weza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati mi niko jukwaani naimba. Kuwapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini. Ukiachilia mbali vipigo.Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu.Ushahidi ninao. .....niliwahi mkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. bado kupigana na kuwatusi wateja pia.Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso. Unazungumziaje suala hili?