Machapisho

Kipute cha R.Madrid, Juventus,liverpool kupigwa leo ratiba nzima iko hapa

Picha
Liverpool wako kwenye uwanja Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya itaendelea leo usiku kwa michezo nane kupigwa kwenye viwanja tofauti. wao wa Anfield wakiwa na kazi moja tu ya kuifunga Fc Basel, katika Mechi yao ya mwisho ya kundi B ili kufuzu kuingia raundi ya Mtoano ya kumi 16 bora. Usiku huu makundi A hadi D ndio yanacheza Mechi zao za mwisho na tayari Timu 11 zimeshafuzu kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 16,na Jumatano ndio Mechi za mwisho za Makundi zitachezwa ambazo zitatoa Timu 5 zilizobakia za kufuzu . Nafasi hizo 5 zinagombewa na Timu 11 na miongoni mwao zipo Klabu za Manchester City na Liverpool, huku wenzao Chelsea na Arsenal tayari wameshasonga. KUNDI A Juventus v Atletico Madrid Olympiakos v Malmö FF KUNDI B Liverpool v FC Basel Real Madrid v Ludo Razgrad KUNDI C Benfica v Bayer Leverkusenn Monaco v Zenit Saint Petersburg KUNDI D Borussia Dortmd v Anderlecht Galatasaray v Arsenal

Hii ndiyo Dawa' ya mpango wa uzazi kwa wanaume

Picha
Mmea wa Gendarusa ambao unasemekana kuzuia wanaume kuzaa Wanasayansi wanadai kuwa dawa mpya iliyozinduliwa ya mpango wa uzazi kwa wanaume imefanikiwa kwa asilimia 99. Dawa hio imetengezwa kutoka kwa mmea ujulikanao kama Gendarusa ambao wanaume wa kisiwa cha Papua wamekua wakitumia kujizuia kuwashikisha wake zao mimba. Mmea huo unasemekana kuwa na madini ambayo yanatatiza uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha kwa kuzimaliza nguvu na pia kuzifanya kutoweza kuingia katika mayai ya mwanamke. Profesa Bambang Prajogo, mtafiti mkuu wa mradi huo anasema ana furaha sana kuripoti kwamba dawa hio itaanza kuuzwa mwaka 2016 baada ya miaka mingi ya utafiti na majaribio. Ingawa dawa hio ya mpango wa uzazi kwa wanaume ina athari zake, kama vile wanaume kuongeza uzazi wanapoitumia wanasayansi wanaamini kuwa athari hizo ni ndogo sana ikilinganishwa na dawa zinazotumiwa na wanawake kwani hauthiri sana homoni zao. Dawa hio inaweza kumezwa saa moja tu kabla ya tendo la n...

Pistorius:Kiongozi wa mashitaka akata rufaa

Picha
Jaji mmoja nchini Afrika Kusini, ameahirisha uamuzi wake ikiwa ataruhusu mwendesha mashtaka kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Pistorius Jaji huyo Thokozile Masipa, aliahirisha kesi hiyo hadi siku ya Jumatano, akisema anataka muda zaidi kuchunguza tetesi zilizowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka ukitaka mahakama imuongfeze adhabu Pistorius. Mwendesha mashtaka Gerrie Nel aliiambia mahakama hiyo kuwa hukumu hiyo aliyopewa Pistorius ni ndogo sana. Oscar Pistorius huenda akaachiliwa huru kutoka gerezani baada ya miezi kumi tu huku akitarajiwa kutumikia kifungo kilichosalia nyumbani. Alifungwa jela miaka mitano mwezi Oktoba kwa kosa la mauaji bila ya kukusudia na siku ya Jumatano mwendesha mashitaka atafahamu ikiwa anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Pistorius au la. Pistorius alijipata matatani baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, mwaka jana. Kiongozi wa mashitaka pia anataka kupinga hukumu ya mauaji dhidi ya Pistorius. Pistorius mwenye ulemavu wa migu...

Picha 4 za mshindi wa Bajaji wa shindano la Tutoke na Serengeti

Picha
Meneja Mauzo  wa Serengeti Breweries Ltd  Mkoa  wa Morogoro Bw.Moses Bartazary (Mwenye kofia ) akikabidhi Funguo ya Bajaj Limo yenye uwezo wa kubeba abiria saba kwa  mshindi  wa kwanza wa shindano  la Tutoke  na  Serengeti  Bi Rukia Almas ambaye ni mkazi wa Kihonda na mfanyakazi  katika Bar ya  Kambarage iliyopo manispaa  ya  Morogoro. Kampeni ya Tutoke na Serengeti wameungana na B-Pesa wataalam wa teknolojia mpya ambao hivi karibuni wamezindua mfumo mpya wa usafirihaji wa fedha. B-Pesa watahusika pia katika kusambaza fedha kwa washindi mbalimbali kote nchini kupitia simu za mkononi.Ili kushinda, unachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Serengeti Premium Lager na angalia chini ya kizibo atakuta namba ambazo zinatakiwa kutumwa kwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenda namba 15317 ili kuingia katika droo. Bi Rukia Almasakionyesha ufunguo wake Mshindi Bajaj aina ya Limo yenye uwezo wa kubeba abiria saba, Bi Ruk...

Miaka 60 jela kwa kutorosha twiga

Picha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro leo imemhukumu miaka 60 jela, mshitakiwa wa kwanza raia wa Pakistani, Kamran Ahmed na kuwaachia huru Watanzania watatu katika kesi ya utoroshaji wanyama hai 153 wakiwemo twiga wanne. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo, amesema baada ya upande wa jamhuri kufanikiwa kujenga kesi dhidi ya Mpakistani huyo kwa kiwango kisicho na shaka, mahakama hiyo imeridhika kwamba alitenda makosa yote manne yaliyowasilishwa dhidi yake. Kobelo amedai mahakama hiyo pia inaawachia huru Watanzania watatu, Hawa Mang’unyuka, Mathew Kimathi na Michael Mrutu kwa sababu upande wa jamhuri imeshindwa kujenga kesi dhidi yao na hata ushahidi uliowasilishwa hauoneshi kuwaunganisha washitakiwa hao moja kwa moja na kosa la kusafirisha wanyama hai nje ya nchi.     Katika hukumu hiyo, Kamran, alikutwa na makosa manne, kushiriki na kula njama ya kutenda uhalifu kinyume cha kifungu 57 (1), sehemu ya 4(1), sura ya kwanza ya kosa l...

Picha 10 za makabidhiano ya maktaba kati ya Shule ya Makumbusho na Read International

Picha
Faraja Kotta Nyalandu akikata utepe leo kwenye makabidhiano ya Maktaba kwenye shule ya Sekondari ya Makumbusho ya jijini Dar es salaam,kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Deogratias Haule,anaefata ni Afisa Elimu sekondari manispaa ya Kinondoni Omath Sanga na Mkurugenzi wa Read International Montse Penjuan, Maktaba hiyo imefadhiliwa na Shirika la Read International ambalo limenunu vitabu vyenye thamani ya fedha za kitanzania milioni 5,Kwa kushirikiana na International School of Tanganyika(IST) ya Dar es salaam ambayo wao wametengeneza mwonekano wa maktaba hiyo kama viti,meza na kabati. Mwonekano wa mbele wa maktaba hiyo kwa ndani mara  baada ya kukabidhiwa rasmi,kwa mkuu wa shule hiyo ya Makumbusho Deogratias Haule. Upande wa pili wa maktaba hiyo. Madaftari yatakayotumika kwaajili ya Kuweka kumbukumbu mbalimbali za Watumiaji wa Maktaba hiyo wanaokuja kuazima na kujisomea. Faraja Kotta ambaye pia anatarajia kuiunganisha shule hiyo na mfumo wa Shule Direct ambao yeye ndiye mwasis...

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Picha
ilipoishia Mazungumzo yao yaliendelea, wakafika nyumbani kwa mwalimu Magdalena, wakapitiwa na usingizi, kutokana na uchovu waliokuwa nao mwalimu Magdalena na mwalimu Joka wakajikuta wakiamka saa 4 asubuhi, tena baada ya John kuwagongea kutokana na kutomuona mwalimu Magdalena shuleni. “Sasa itakuwaje, nje kuna hodi inagongwa na sauti ya huyo mtu namjua ni wa shuleni, kama akikuona itakuwa balaa upya, watahisi kuna kitu kimefanyika kati yangu na wewe, sasa naomba ujifiche humu humu ndani mi natoka kumsikiliza.’’ “Sawa.” sasa endelea Mwalimu Magdalena alipotoka nje akakutana na John, mwanafunzi anayempenda, John hakutaka kuhoji chochote hadi aingie ndani lakini mwalimu Magdalena alionyesha hofu kama ya kusita, lakini akakubaliana na yote, John akaingia akakaa kitandani huku mwalimu Joka akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda cha mwalimu Magdalena. “Mwalimu mbona hadi sasa hujafika shuleni kila mtu anahofu nawe, hakuna anayeelewa somo lolote hadi wakuone, mwa...