Machapisho

Marekani yashindwa kukomboa raia wake Syria

Picha
Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo hivi karibuni lilifanya operesheni ya anga na nchi kavu ili kuwakomboa Wamarekani waliotekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Daesh nchini Syria lakini  halikufanikiwa. Msemaji wa Pentagon Admiral John Kirby ameeleza kuwa, operesheni hiyo haikufanikiwa kwani mateka hawakuwepo katika eneo walilolilenga. Imeelezwa kuwa, Rais Barack Obama ndiye aliyeamuru operesheni hiyo ya siri iliyofeli nchini Syria ili kuwakomboa Wamarekani wanaoshikiliwa na kundi la Daesh akiwemo mwandishi habari James Foley aliyechinjwa na kundi hilo. Matamshi hayo yametolewa na maafisa wa Marekani siku moja baada ya kundi la ISIL kutoa video inayoonesha mwandishi habari James Foley akikatwa kichwa. Hata hivyo Rais Barack Obama amesema kuwa, Marekani itaendelea kufanya kila iwezalo kuwalinda raia wake akidai kwamba  kukatwa kichwa mwanahabari huyo kumethibitisha kuwa kundi la Daesh halina dini. Ikumbukwe kuwa kun...

Sudani waomba muafaka

Picha
Marais wa Sudan na Sudan Kusini wamesisitiza juu ya azma ya nchi zao ya kupatiwa ufumbuzi matatizo yaliyopo kati ya nchi hizo mbili. Marais Omar Hassan al-Bashir na Salva Kiir wamesisitiza hayo katika mazungumzo yao waliyoyafanya kwa njia ya simu na kueleza kwamba, wanataka matatizo yaliyopo kati ya Juba na Khartoum yapatiwe ufumbuzi. Rais Omar al-Bashir amesisitiza katika mazungumzo hayo kwamba, Khartoum inataka amani na uthabiti upatikane katika nchi jirani ya Sudan Kusini. Wakati huo huo, Abdul Rahman Muhammad Hussein, Waziri wa Ulinzi wa Sudan ametoa wito wa kuharakishwa utekelezwaji wa makubaliano ya usalama yaliyotiwa saini kati ya Khartoum na Juba Disemba mwaka 2012 huko Addis Ababa, Ethiopia. Tangu Sudan Kusini ilipojitenga na Sudan na kujitangazia uhuru wake Julai 9 mwaka 2011 imekuwa ikivutana na jirani yake huyo kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo la mipaka-Chanzo iran swahili

Watoto wazidi kutumiwa vitani Sudan

Picha
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa, idadi ya watoto wanaotumikishwa vitani nchini Sudan Kusini imeongezeka kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya jeshi la serikali na waasi. Mkurugenzi Mtendaji wa HRW barani Afrika Daniel Bekele amesema kwamba, jeshi la Sudan Kusini limeanza tena hatua zisizofaa za kuwatumikisha vitani watoto na kwamba raia na viongozi wa kijeshi wanapaswa kuwaondoa watoto vitani na kuwarejesha katika familia zao haraka iwezekanavyo. Kwa mujibu wa Human Rights Watch waasi pia wanawatumisha kwa lazima watoto vitani. Kuanzia mwezi Disemba mwaka jana, Sudan Kusini ilitumbukia katika machafuko baada ya kuzuka mapigano kati ya askari watiifu kwa Rais Salva Kiir wa nchi hiyo na makamu wake wa zamani Riek Machar katika mji mkuu Juba. Mgogoro huo uligeuka vita vya ndani na kusababisha vifo vya watu wengi huku wengine wakilazimika kuwa wakimbizi.-Crdt iran swahili

Waandamanaji wataka Nawaz Sharif ajiuzulu

Picha
Waandamanaji wanaotaka waziri mkuu Nawaz Sharif ajiuzulu. Islamabad, Pakistan Aug. 19, 2014. Jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano. Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano. Maelfu ya waandamanaji wanopinga serikali wamekuwa katikati ya mji mkuu wa Pakistan kwa karibu wiki moja, katika juhudi za kumshinikiza waziri mkuu Nawaz sharif kujiuzulu. Wote serikali na viongozi wa maandamano hayo hawaelekei kurudi nyuma, na hivyo kuongeza hofu ya mapambano baina ya polisi na waandamanaji hao kila kuchao. Mwanasiasa wa upinzani Imran Khan na kiongozi mashuhuri wa kidini Tahir-ul Qadri, wameaanda maandamano ya umma, ingawa si kwa ushirikiano lakini wana...

Kagame aapa kupambana na biashara ya binaadamu

Picha
Rais Paul Kagame wa Rwanda. Biashara haramu ya binaadamu inazidi kuongezeka Rwanda, huku Rais Paul Kagame wa nchi hiyo akikiri vijana, hasa wasichana, wamekuwa wakiuzwa kama bidhaa katika nchi jirani na hata mashariki ya mbali.  Biashara ya kuuza watu imekuwa ni kama haijulikani hapa Rwanda lakini tatizo hilo limeibuka kuwa tishio miaka ya hivi karibuni ijapokuwa chini kwa chini. Na sasa limechukua sura mpya baada ya Rais Kagame kulizungumzia, akisema kwamba kwa hatua lilikofikia haliwezi kuvumiliwa tena na hivyo ngazi za usalama hazina budi kuchukua hatua zaidi ya ilivyo sasa. "Nimekuwa nikisoma ripoti na taarifa kuhusu watoto wetu hasa wale wa kike ambao wamebadilishwa kama bidhaa na kuuzwa,inakuwaje mambo haya yanafanyika! Yaani mtu anauzwa tu kama kitu cha kawaida tena sisi kama viongozi tukifahamu wazi kuwepokwa tatizo hilo. Hapa linapaswa kukoma." Alisema Rais Kagame katika hafla maalum ya kuwaapisha wajumbe wa baraza la mawaziri siku ya Jumatatu. A...

Alama ya ulaji ndizi yamponza Tavecchio

Picha
Carlo Tavecchio raisi wa shirikishoa la soka Italia ,lawamani Shirikisho linalo simamia mpira wa soka ulaya,UEFA linania ya kumchunguza rais wa soka aliyechaguliwa wa shirikisho la soka huko Italia Carlo Tavecchio . Tavecchino anashutumiwa pia kushukiwa alionesha ishara ya ubaguzi wa rangi wakati wa harakati za kampeni zake. Kutokana na madai hayo, Tavecchio amekwisha omba radhi kwa kitendo hicho cha ishara ya kula ndizi, kitendo kinachojulikana kimataifa katika soka kama ishara ya ubaguzi wa rangi. Hata hivyo msamaha wake umegonga mwamba na kushindwa kuzuia harakati zinazo endelea ,dhidi ya nafasi yake ya urais na hivyo kujitia kikaangoni,je atajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe? Ama atachomoka kwenye fitina hii? Tusubiri uchunguzi .

Ofisi za NFF abuja zateketea

Picha
Moto wateketeza ofisi za NFF Abuja Moto mkubwa umetekeza makao ya shirikisho la soka la Nigeria NFF iliyoko Abuja. Iliwachukua zaidi ya saa mbili kwa zima moto wakisaidiana na umma kuuzima moto huo mkubwa . Afisa wa kuzima moto Eyo Ime ameiambia BBC kuwa wanashuku chanzo cha moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme. Katibu mkuu wa NFF bwana Musa Amadu amesema kuwa moto huo ulianzia katika afisi ya mhasibu wa shirikisho hilo. "Niliwasili kama kawaida lakini nikakatazwa kupanda ghorofa kwani tayari moshi ulikuwa unafuka '' "Wafanyikazi wa shirikisho hilo wangeweza kuzima moto huo lakini walishindwa kuingia ofisini humo na hivyo hawangfeweza kubaini chanzo kikamilifu'' ''Hata hivyo nashukuru mungu kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha yake kutokana na moto huo kwahivyo hakuna faida ya kumlaumu mtu yeyote'...