Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2021

Alexei Navalny akamatwa baada ya kurejea nyumbani

Picha
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas ametoa mwito hii leo wa kuachiliwa kwa Alexei Navalny, mkosoaji mkuu wa rais wa Urusi Vladimir Putin, anayeshikiliwa kizuizini baada ya kurejea nchini humo jana akitokea Ujerumani.  Maas amesema Urusi inapaswa kuheshimu majukumu yake ya kulinda haki za raia na utawala wa sheria, ambayo pia yanamhusisha mkosoaji huyo mwenye ushawishi mkubwa. Matamshi yake yanakwenda sambamba na yaliyotolewa na viongozi wa nchi nyingine za Ulaya na Marekani.  Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa rais mteule wa Marekani Joe Biden, Jake Sullivan amesema hatua hiyo ya Urusi sio tu ukiukaji wa haki za binadamu, lakini pia ni dharau kwa watu wa taifa hilo wanaotaka sauti zao zisikike.  Mawakili wa Navalny wanasema hawajaruhusiwa kumuona tangu alipokamatwa jana. Urusi imesema ukosoaji wa nchi za magharibi una lengo la kuficha matatizo ya ndani ya nchi hizo.