Wafuasi wa dhehebu wauawa Angola
![]() |
Angola |
Wanachama kadha wa dhebu moja lililojihami wameuawa kwenye mapigano na vikosi vya usalama nchini Angola.
Chama
kikuu cha upinzani nchini humo cha UNITA kilisema kuwa huenda watu 200
waliuawa huku chama tawala cha MPLA kikisema kuwa ni watu 13 waliuawa.
UNITA
kinaitaka serikali ya Angola kuchunguza vifo vya waumini wa dhebu la
Seventh Day Light of the World ambalo lilijitenga kutoka kanisa la
Seventh Day Adventist.
Dhehebu hilo linamini kuwa dunia itaisha
mwishoni mwa mwaka huu na limetoa witu kwa wafuasi wake kuondoka makwao
na kuelekea milimani.
bbc
Maoni
Chapisha Maoni