TRA kutoa elimu,sheria ya kodi
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema inajipanga kutoa
elimu ya ulipaji kodi na sheria za kodi kwa wajasiliamali pamoja na wafanyabiashara
wengine kutoka nje ya nchi ili waweze kutambua umuhimu wake.

Afisa Mkuu katika Idara ya Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi
(TRA), Yeremiah Mbaghi, alisema kila mwaka wamekuwa na kawaida ya kukutana na
wafanyabiashara kutoka China kwa lengo la kuwaelimisha masuala ya ukusanyaji
kodi pamoja na sheria za kodi kutokana na kuwa sheria za nchi hizo mbili zinatofautiana.
Mbaghi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya
elimu ya kodi iliyowashirikisha wafanyabiashara
na wawekezaji kutoka China.
“Tutakuwa tunatoa elimu
ya kodi kwa wajasiliamali mbalimbali wa ndani, wafanyabiashara wa nje pamoja na wawekezaji lakini leo ni zamu
ya wachina na tutakuwa tunatoa kwa siku maalumu kwa kila sekta tofauti,”
alisema Mbaghi.
Naye Mshauri wa Kisiasa katika Ubalozi wa China, Li Xuhang,
amewataka wafanyabiasha na wawekezaji kutoka China kuhudhuria semina za elimu
ya ulipaji kodi zinazotolewa na TRA kwa lengo la kujifunza.
Aidha aliwataka kulipa kodi kwa hiyari pamoja na kufuata
sheria zake.
Maoni
Chapisha Maoni