Siku tatu za maombolezo Ethiopia zaanza
![]() |
Islamic State wakienda kuwaua raia wa Ethiopia |
Ethiopia imeanza siku tatu za
maombolezi ya kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na wanamgambo
wa kundi la Islamic State nchini Libya.
Bendera zitapepea nusu
mlingoti wakati nalo bunge la nchi hiyo likikutana kujadili hatua ambazo
litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya ishirini.
Msemaji
wa serikali Redwan Hussein, alisema kuwa waathiriwa hao wanaaminika
kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani ulaya.
Mungano
wa Afrika ambao una makao yake makuu nchini Ethiopia ulilaani mauaji
hayo na kusema kuwa utafanya mikakati ya kuhakikisha kuwepo usalama
nchini Libya.
Wanamgambo wa Islamic State walitoa kanda ya video
ambayo inakisiwa kuonyesha mauaji hayo yanayoonyesha watu hao wakipigwa
risasi na kukatwa vichwa.
Maoni
Chapisha Maoni