Nyota wa ligi ya NBA kukipiga Afrika
![]() |
Luol Deng |
Chama cha Mpira wa Kikapu cha
Marekani, NBA kimetangaza Jumatano mipango ya kucheza mchezo wake wa
kwanza barani Afrika, katika mchezo wa mwezi Agosti ambao
utawashirikisha wachezaji wa mpira wa kikapu barani Afrika katika
jitihada za kuufanya mchezo huo kupata mashabiki duniani.
Mechi ya
Agosti Mosi mjini Johannesburg itaundwa na timu ya Afrika "Team Africa"
ikiwashirikisha wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa ligi ya NBA wa
kizazi cha kwanza na cha pili kutoka Afrika dhidi ya timu ya dunia"Team
World,"ambayo itakuwa na wachezaji kutoka maneo mengine duniani.
Mchezaji
nyota mara mbili wa NBA All-Star, Luol Deng wa timu ya Miami Heat,
ambaye alizaliwa katika nchi ambayo kwa sasa ni Sudan Kusini, ataongoza
timu ya Team Africa, wakati nyota mara nane wa NBA Chris Paul wa Los
Angeles Clippers atakuwa nahodha wa timu ya Team World.
Tangazo
hilo limetolewa wakati ligi ya Marekani imetangaza kalenda yake ya mwaka
kwa michezo ya nje kwa mwaka 2015-2016. NBA tayari imetangaza michezo
nchini Brazil, China na Mexico.
![]() |
Chris Paul |
Muundo wa mchezo wa Afrika unatofautiana kwa kiasi kikubwa na
mashindano mengine ya nje ya NBA, ambayo inahusisha timu mbili za NBA au
mchezo wa kabla ya msimu.
Uwanja wa Johannesburg, Ellis Park
Arena, wenye viti 6,300, unaonekana kuwa mdogo zaidi ya viwanja kama O2
mjini London na Ulker Sports Arena mjini Istanbul, Uturuki ambavyo
vimewahi kuwa wenyeji wa michezo ya msimu wa 2014-15.
Sal LaRocca,
rais wa shughuli za kibiashara duniani wa NBA, amesema ligi hiyo "bado
iko katika hatua ya mwanzo kabisa" ya kuendeleza Afrika kuwa soko la
mpira wa kikapu.
"Kila eneo tulimoanzisha biashara yetu, kwa namna moja au nyingine, tulianza na mchezo," LaRocca ameiambia AFP.
"Kwa hiyo hiki ni kigezo muhimu katika maendeleo yetu barani Afrika."
Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa zaidi barani Afrika, na raga una mashabiki wengi nchini Afrika Kusini.
NBA
ina ofisi 12 katika masoko ya kimataifa. Kubwa kuliko yote ni China,
ambako inaajiri kiasi cha watu 130 mjini Beijing, Shanghai, Hong Kong na
Taiwan.
NBA ilifungua ofisi yake mjini Johannesburg mwaka 2010 na
kwamba sasa ina wafanyakazi 11 ambao wanasimamia mipango yote barani
Afrika.
Maoni
Chapisha Maoni