North Mara yaibuka kidedea
KAMPUNI ya madini ya North Mara Gold Mine imeibuka mshindi wa jumla
wa Tuzo za Rais za Huduma za Jamii na Uwezeshaji (CSRE), zilizotolewa kwa Makampuni
yaliyofanya vizuri kwenye ushiriki wa miradi ya kijamii wa mwaka 2014.

Kampuni hiyo pia imefanikiwa kushinda tuzo ya jumla ya Kampuni kubwa
ya Madini baada ya kuonekana kuchangia zaidi miradi mbalimbali katika sekta za elimu,
afya, miundombinu na ajira.
Akizungumzia wakati akikabidhi tuzo hizo jijini Dar es Salaam ,
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal amesema tuzo hizo zina lengo la
kuwahamasisha wawekezaji kurejesha shukrani kwa jamii inayozunguka migodi hiyo.
Bilal alisema kuwa kila mwaka shindano hilo limekuwa likiboreshwa
hali iliyochangia kuvutia kampuni nyingi kushiriki tofauti na mashindano ya
mwaka jana ambapo kampuni zilizoshiriki zilikuwa 38 lakini mwaka huu idadi
imeongezeka na kufikia 59.
Naye Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizungumzia
tuzo hizo amesema serikali imedhamiria kuwawezesha wawekezaji wa Madini
kuwafaidisha wananchi wa maeneo wanayoishi kwa kuwaajiri au kununua bidhaa zao.
“Wananchi wanaokuwa wanazunguka migodi hiyo wanahitaji kuona
wanajengewa barabara nzuri, wanajengewa hospitali nzuri, wanafunzi wanapata
madawati, shule nzuri, kwani hivyo ni vitu vya msingi kufanyika hivi sasa.
“Kwa sasa tumefikia wakati wa kuwawekea sheria na taratibu ambazo
zitawasaidia kujua vigezo vinavyohitajika kupata ushindi,” amesema.
Kampuni nyingine zilizopata Tuzo ya Kampuni ndogo za Madini (Busolwa
Mining Limited), Kampuni ya uzalishaji wa mafuta na gesi (Songas), Kampuni ya
utafutaji wa mafuta na gesi (Afren Tanzania).
Tuzo nyingine ya Utafutaji wa Madini (Mantra Tanzania Limited), Tuzo
ya Kampuni ya kati ya Madini (Shanta Mining (T) Limited), Kampuni kubwa ya
Madini (North Mara Gold Mine).
Tuzo nyingine maalumu zilizotolea ni msaada wa Sekta ya Elimu ya
Sekondari (Geita Gold Mine Limited), Elimu ya Juu (Statoil Tanzania) na
Miundombinu (Buzwagi Gold Mine)
Maoni
Chapisha Maoni