Majambazi yaua wafanyakazi Bonite
WATU wawili wamefariki
dunia mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, baada
ya kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa
majambazi.
Wakati wa tukio hilo,
majambazi hao walipora mamilioni ya fedha, mali ya Kampuni ya Bonite ya mjini
Moshi.

Mkuu wa Wilaya ya
Moshi, Novatus Makunga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea
juzi saa 12 jioni katika eneo la Kili FM Soweto.
Kwa mujibu wa mkuu huyo
wa wilaya, tukio hilo lilitokea wakati watu hao wawili walipokuwa wakirudi
ofisini kutoka kwenye mauzo mitaani.
“Wafanyakazi wa Bonite walikuwa wakitoka kukusanya mauzo
ya kampuni hiyo katika kituo cha Himo, stendi ya mabasi Moshi, Kiusa na
Kiboriloni.
“Wakati huo, walikuwa kwenye
gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 803 ATR na walipofika eneo la
Soweto, walivamiwa na majambazi hao,” alisema Makunga.
Alisema majambazi hao, walikuwa wanne na kwamba wakati
wanawavamia wafanyakazi hao walikuwa wamepanda pikipiki mbili.
“Pia, majambazi hao
walikuwa na bastola na walipolifikia gari la wafanyakazi wa Bonite, walilivamia
na kuanza kumimina risasi na kumpiga mlinzi wa kampuni hiyo kichwani na
kufariki papo hapo pamoja na dereva ambaye naye alifariki baada ya kupigwa
risasi kifuani.
“Baadaye, majambazi
walipora fedha walizokuwanazo na kutokomea kusikojulikana,” alisema.
Aliwataja marehemu hao,
kuwa ni mlinzi Edson Shamba, (56), aliyekuwa na bunduki aina ya Shortgun
yenye namba 8710653.
Mwingine ni Amin
Mselem, (61), mkazi wa Mtaa wa Chunya, Manispaa ya Moshi.
“Pamoja na hayo, maofisa
mauzo wa kampuni hiyo waliokuwa kwenye gari hilo hawakujeruhiwa na
wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
“Kutokana na tukio
hilo, vyombo vya ulinzi tayari vimeshaanza uchunguzi wa kina na tunawaomba wananchi
watoe ushirikiano ili wahusika waweze kukamatwa haraka,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Maoni
Chapisha Maoni