Liverpool yasaini mkataba mpya wa udhamini
Mabingwa wa zamani wa England na ulaya Liverpool wamesaini upya
mkataba wa udhamini na benki ya Standard Chartered kwa miaka mitatu
zaidi baada ya mkataba wa awali kufikia mwisho .

Liverpool na benki hiyo wamekuwa washirika kwa muda wa miaka mitano
tangu waliposaini mkataba wa kwanza mwaka 2010 na chapa ya benki hiyo
imekuwa kwenye jezi ya Liverpool kwa miaka mitano sasa.
Vipengele vya mkataba huo havijawekwa wazi lakini magazeti ya michezo
ya kila siku nchini England yameripoti kuwa thamani halisi ya mkataba
huo ni paundi milioni 20 kwa msimu nah ii inamaanisha kuwa Liverpool
italipwa jumla ya paundi milioni 60 kwa muda wote wa mkataba huo.
Taarifa hizi za kuongezwa kwa mkataba wa udhamini toka kwa Standard
Chartered zitakuwa muziki masikioni mwa mashabiki wa klabu hiyo katika
kipindi hiki ambapo kocha Brendan Rogers anapiga mahesabu ya kufanya
usajili ili kuimarisha kikosi chake baada ya msimu ambao haujawa na
mafanikio .
Maoni
Chapisha Maoni