Jeshi laapa kupambana na Boko Haram
![]() |
Msemaji wa jeshi (Chris Olukolade) |
Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa
linafanya oparesheni ya mwisho kwenye msitu moja ambao unaaminiwa kuwa
ngome kuu ya wanamgambo wa Boko Haram.
![]() |
Boko Haram |
Serikali
ya Nigeria inasema kuwa Boko Haram wako mbioni na jeshi limeapa
kuwashinda kabla ya kuapishwa kwa rais mpya Muhammadu Buhari tarehe 29
mwezi Mei.
Inaaminika kuwa zaidi ya wasichana 200 wa shule ambao
walitekwa nyara mwaka mmoja uliopita kutoka mji wa Chibok huenda
wameshikiliwa ndani ya msitu huo-chanzo bbc
Maoni
Chapisha Maoni