HONDA yawatia matatani
WAKAZI wawili Jijini Dar es Salaam, Gift Norah (26) na
Hassan Abeid (20) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya
Kinondoni wakikabiliwa na shtaka la kuiba pikipiki yenye thamani ya Sh
milioni 2.3
Mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Wakili wa Serikali
Zawadi Mdegela, amedai kwamba tukio hilo lilitokea Machi 17 mwaka huu eneo la
Mbezi Beach Wilayani hapo.

Zawadi aliongeza kuwa watuhumiwa hao waliiba pikipiki
yenye namba za usajili T. 818 CQH HONDA inayomilikiwa na Joseph Njuu.
Watuhumiwa baada ya kusomewa shtaka hilo wamekana kosa
hilo na upelelezi bado unaendelea ambapo Hakimu Kiliwa alisema dhamana kwa
watuhumiwa iko wazi kisheria hivyo aliwataka waje na wadhamini wawili walioajiriwa
serikalini ama katika taasisi yoyote inayotambulika kisheria.
Shauri hilo limeahirishwa hadi Mei 6 mwaka huu na
watuhumiwa walirudishwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Maoni
Chapisha Maoni