Covenant Benki yaipiga tafu Namtumbo
BENKI ya Covenant ya jijini Dar es salaam imetoa msaada wa saruji
yenye thamani ya Sh milioni 2.5 kwa ajili ya umaliaziaji wa ujenzi wa maabara
katika Shule ya Sekondari ya Msindo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Sabetha Mwambeja alisema msaada huo ni
utekelezaji wa sera yao ya kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii.
Amesema Conenant benki ina program za kusaidia shughuli za kijamii
hususani katika sekta zisizokuwa rasmi pamoja na vijana kwa kuwezesha
upatikanaji na uwezeshaji wa masomo kwa njia moja au nyingine.
Naye Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Margareth Kyarwenda amesema benki
inatambua masomo ya sayansi ni muhimu katika nchi na maabara ni sehemu ya
maandalizi ya wataalam wa fani hiyo.
“Tunatambua BRN (Mpango wa Matokeo Makubwa sasa) kwa kiasi kikubwa
inategemea sayansi na teknolojia hivyo benki ipo mstari wa mbele kuhakikisha
nchi inasomesha na inakuwa na wataalam wa kutosha kupitia shule hizi” amesema
Margareth.
Akipokea msaada huo, Diwani wa Kata ya Msindo, Mohammed Birika amesema mchango huo niwa pili kwa shuele hiyo ambapo awali benki hiyo ilisaidia
ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi ya utawala katika shule hiyo.
“Tunashukuru msaada wa benki hii kwani umechangia kwa kiasi kikubwa
ufaulu wa wanafunzi katika shule yetu ya Msindo ambapo kila mwaka wanafunzi
wanafaulu na kuendelea kidato cha sita katika sehemu mbalimbali nchini”amesema
Birika
Maoni
Chapisha Maoni