Pluijm aibua mapya Yanga
KOCHA Mkuu wa Yanga,
Hans van der Pluijm, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kusaka mikanda ya video za
wapinzani wao wajao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, FC Platnum ya
Zimbabwe.
Yanga Ijumaa
iliyopita ilitinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya kuitoa BDF XI ya
Botswana katika raundi ya awali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2.

Katika mchezo wa
kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga walishinda
mabao 2-0 kabla ya kulala kwa mabao 2-1 ugenini Ijumaa iliyopita.
Katika raundi
inayofuata, Yanga watakutana na FC Platnum iliyoitoa Sofapaka ya Kenya.
Kwa kufahamu ugumu
wa mchezo huo, Pluijm ameanza kujipanga mapema kuhakikisha anawatoa Wazimbabwe
hao na kusonga mbele, hicho kikiwa ndicho kipaumbele chake, kuhakikisha Yanga
inafanya kweli katika soka la kimataifa.
Akizungumza na
BINGWA jana kabla ya safari ya kurejea nchini Tanzania, Pluijm alisema akipata
mikanda ya kama 10 ya wapinzani wake wajao, hatakuwa na sababu ya kushindwa
kuwatoa kwenye michuano hiyo.
“Nataka kuwasoma
zaidi kuona ni vipi ninaweza kuwaandaa wachezaji wangu kupambana nao, sina
wasiwasi na timu yangu, kwa sasa imeiva na mchezo wetu wa juzi (Ijumaa) wa
ugenini, umetusaidia sana kwani wachezaji wangu wamejifunza mambo mengi,
ikiwamo kukabiliana na wapinzani ugenini,” alisema Mholanzi huyo.
Kikosi cha Yanga
kinatarajiwa kutua nchini leo kutoka Botswana na kwamba baada ya kuwasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kitakwenda moja kwa moja
Bagamoyo kujichimbia kuiwinda Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
utakaopigwa wikiendi hii.
Mchezo huo dhidi ya
Simba unatarajiwa kuwa na msisimkoa wa aina yake kwani timu zote mbili
zimeonekana kupania kutoka uwanjani na ushindi.
Kwa upande wao,
Simba walitarajiwa kuondoka Dar es Salaam jana kwenda kuweka kambi Zanzibar,
kama sehemu ya maandalizi ya kuwaangamiza Yanga.
Katika mzimamo wa
ligi hiyo, Yanga wapo kileleni na pointi zao 31, wakati Simba inashika nafasi
ya tatu kwa pointi 24, ikiwa imecheza mechi moja zaidi ya watani wao hao wa
jadi. -bingwa
Maoni
Chapisha Maoni