Goran: Wembe ni ule ule Tanga
BAADA ya kuibuka na ushindi mara tatu mfululizo, Kocha
Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, amesema wembe ni uleule katika mchezo wao wa
kesho dhidi ya Maafande wa Mgambo JKT.
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao, Simba, tayari
kimeshawasili jijini Tanga kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kesho Uwanja wa
Mkwakwani.
Akizungumzia mchezo huo, Goran alisema amefanya
maandalizi mazuri katika kikosi chake, huku akiwapa majukumu wachezaji wake
kuhakikisha wanarudi jijini Dar es Salaam wakiwa na pointi tatu mkononi.

Alisema ametumia siku mbili kwa ajili ya kufanyia
kazi kasoro zilizojitokeza katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, hivyo
tayari kikosi chake kipo imara kuwavaa Mgambo.
“Kila mtu anafahamu jukumu lake, tumepata ushindi
katika mchezo dhidi ya Mtibwa, hivyo pia tunakwenda kwa wapinzani wetu tukiwa
na akili ya kutaka kupata ushindi,” alisema.
Goran alisema anatambua anakutana na timu ngumu
na kutumia vyema uwanja wa nyumbani, lakini kwa upande wake atahakikisha vijana
wake wanatimiza majukumu aliyowapa.
“Kila mmoja anatambua jukumu lake, kwa hali hiyo
tayari nimeshaandaa kikosi cha ushindi kwa kufikia malengo ya timu kumaliza
katika nafasi za juu au kutwaa ubingwa,” alisema kocha huyo.-bingwa
Maoni
Chapisha Maoni