Tanzania, Ufaransa waanzisha kundi la kirafiki
UBALOZI wa Ufaransa nchini umeanzisha kundi la
kirafiki kati ya Tanzania na Ufaransa, kwa ajili ya kubadilishana uelewa katika
masuala mbalimbali ikiwemo siasa, sayansi, utamaduni na uchumi.
Balozi wa Ufaransa nchini, Bertha Semu-Somi, alisema
hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mjini Dar
es Salaam.

Alisema kikundi hicho kitazinduliwa rasmi Februari
20, mwaka huu nyumbani kwa balozi na kwa kuanzia kitakuwa na wajumbe 50 ambapo
baadaye wataendelea kuongezeka.
“Wajumbe wa kikundi watakuwa wanakutana mara tatu
kwa mwaka kwa ajili ya kubadilishana mawazo na ujuzi, ajenda mbalimbali
zitajadiliwa zikiwemo za kisiasa, elimu na uchumi.
Alisema wapo Wafaransa wanaohitaji kuijua zaidi
Tanzania na wapo Watanzania wanaohitaji kujua utamaduni wa Wafaransa, hivyo
kupitia kikundi hicho kila upande utanufaika.
“Lengo ni kuunganisha watu tofauti tofauti, kundi
litakuwa uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume wa Kitanzania na Ufaransa kwa
ajili ya maendeleo,”-MTANZANIA
Maoni
Chapisha Maoni