Mbeya City yapangua adhabu ya TFF kwa Nyosso
KOCHA Mkuu wa kikosi cha Mbeya City, Juma Mwambusi, ni kama
amepinga adhabu aliyopewa beki wake, Juma Said ‘Nyosso’ na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), baada ya kusema ni kubwa na ni kama wameidhulumu timu.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya TFF kutoa
adhabu ya kumfungia beki huyo kucheza mechi nane kwa kosa la kumshika makalio
straika wa Simba, Elias Maguli.
Nyosso alidaiwa kutenda kosa hilo la udhalilishaji katika
mchezo wao dhidi ya Wanamsimbazi, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam, ambapo wagonga nyundo hao wa Mbeya waliweza kuibuka na ushindi wa
2-1
Mwambusi alisema adhabu aliyopewa
mchezaji wake ni kubwa, kwani ni sawa na kutocheza mechi za mzunguko mzima,
kitu kinachoweza kuigharimu timu.
“Ukweli sijui kanuni gani zimetumika katika hili, ni bora
TFF waziweke wazi, kumsimamisha mchezaji michezo nane ni sawa na mzunguko mmoja,
bora wangemtoza faini ya pesa, huko ni kuua kiwango cha mchezaji mwenyewe
pamoja na kutoitendea haki timu, ukizingatia tulimsajili kwa kipindi kifupi,” alisema
Mwambusi.
Wakati huo huo, uongozi wa wagonga nyundo hao umepanga
kukata rufaa kupiga adhabu iliyotolewa.
Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten, alisema wapo katika
mchakato wa kukata rufaa TFF, kwani maamuzi yaliyotolewa hayakuangalia pande
zote, kwa maana ya mchezaji, timu anayoitumikia na aliyetendewa kosa.
“Kuanzia kesho tutawasilisha rufaa yetu TFF kupinga maamuzi
yaliyotolewa na Kamati ya Maadili, siyo kwamba tunatetea vitendo vya utovu wa
nidhamu, hatukumtuma Nyosso kutendea kosa lile, sasa kumsimamisha mechi nane ni
sawa na kuihukumu timu isimtumie, ni heri angetozwa faini,-bingwa
Maoni
Chapisha Maoni