Algeria na Afrika kusini kushuka dimbani leo
![]() |
Wachezaji wa Afrika kusini wakikabiliana na wenzao wa Misri katika mechi ya dimba la mataifa ya Afrika 2011 |
Algeria yenye wachezaji nyota
Yacine Brahimi, Sofiane Feghouli na Islam Sliman ambao umoja wao
unatakiwa kufahamika kama utatu wa dhahabu wanataka kuanza kwa uimara
michuano hii.
kutokana na uwepo wa wachezaji wenye kiwango cha juu
watu wengi wanaipa Algeria nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo,
lakini kocha Christian Gourcuff amepuuza mtizamo kuwa timu yake ina
nafasi kubwa ya kutwaa kombe.Afrika Kusini wao wanayatoa mashindano hayo kwa kumuenzi Senzo Meyiwa, aliekua nahodha wa timu ya Taifa ambaye aliuawa mwezi Oktoba mwaka jana.
![]() |
Wachezaji wa Algeria |
Naye beki Anele Ngcongca anaamini kwamba licha ya upande wao kutokuwa na wachezaji wenye majina makubwa kutoka ligi za ulaya wana uwezo wa kushindana.
"Kujiamini na morali ya timu iko juu sana,tunataka kwenda huko na kuwahakikishia kuwa Afrika Kusini kuna vipaji.
![]() |
Marehemu Senzo Meyiwa |
Maoni
Chapisha Maoni