Viongozi wa dini washauriwa kwenda shule
VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kwenda shule kusoma masomo ya
kijamii badala ya kung’ang’ani ya kidini pekee hali ambayo husababisha waumini
wengi wasiwe na ufahamu wa kuzijua sheria na haki zao za msingi ndiyo maana
wamekuwa wakionewa na kupoteza haki zao.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mchungaji Anna Suguye wa
huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) ya jijini Dar es Salaam
wakati wa mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika Bungo
Kibaha mkoani Pwani.

Anna ambaye amehitimu Shahada ya Usimamizi wa Biashara na Uongozi wa
Rasimaliwatu alisema ni vizuri viongozi wa dini kusoma masomo ya kijamii ambayo
pia yanaweza kuwasaidia waumini wao kwani watakuwa na uelewa mpana wa
kuwaongoza waumini wao.
“Kuna viongozi wengi wa dini hawajui sheria za kuwaongoza watu
wanaowahudumia na ndiyo maana wamekuwa wakitoa mafundisho ya kuwapotosha watu
wao jambo ambalo ni hatari kwa taifa,”alisema Anna.
Aidha, Anna alisema kwa baadhi ya viongozi wa dini hufikiri kusoma
masomo ja kijamii ni dhambi na badala yake wanang’ang’ana na elimu ya kidini
pekee na kuongeza kwamba kiongozi mzuri ni yule aliyesoma elimu zote mbili kwa
manufaa ya anaowaongoza.
Maoni
Chapisha Maoni