Tohara yaharibu Sherehe za Ukimwi
MAADHIMISHO ya Siku ya Ukimwi wilayani Tarime yalidorora
baada ya wananchi kutofika eneo husika na badala yake kwenda kwenye sherehe za jadi za tohara kwa
wanaume na watoto wa kike.
Tuklio hilo lilitokea Kijiji cha Nyamwaga ambako maadhimisho ya
Ukimwi yalifanyika.
Kutokana na tukio hilo
aliyekuwa mgeni rasmi, Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Tarime, Victir
Kabuje, alisema alisikitishwa na kitendo cha wananchi kutothamini elimu ya
Ukimwi na kukimbilia sherehe za ukeketaji.

Kabuje ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya Tarime, John
Henjewele, aliwaasa wananchi hao kuacha kukeketa wasichana bali tohara ifanyike
kwa wanaume pekee
Hata hivyo Kabuje alimtupia lawama Mwenyekiti wa Kijiji cha
Nyamwaga, Kirigiti Sasi kwa kushindwa
kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi.
Aliwaasa wananchi kuacha mila potofu ili kuendana na wakati.
Maoni
Chapisha Maoni