RC awa mbogo kwa wakurugenzi Mwanza
MKUU
wa Mkoa wa Mwanza, Magessa Mulongo, juzi aliugeuza ukumbi wa
mikutano kuwa mahakama baada ya kuwaweka kiti moto wakurugenzi, mameya,
wenyeviti wa wilaya na watumisshi wengine kueleza sababu ya Jiji la Mwanza
kupata hati chafu ya hesabu na kukithiri kwa migogoro.
Pia
aliwataka kueleza hatua ya utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la
ujenzi wa maabara tatu katika kila shule ya sekondari ifikapo Novemba 30
kitendo ambacho kilifanya baadhi ya watendaji kushindwa kuzungumza.
Mulongo
juzi alipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Kinisaga na niaba ya
aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Evarist Ndikilo aliyehamishiwa Arusha na kukabidhiwa
ofisi hiyo rasmi
![]() |
Magessa Mulongo |
Alianza
kuwasimamisha wenyeviti wa wa kila wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ambazo
ni Ilemela, Nyamagana, Ukerewe, Misungwi, Magu, Sengerema na Kwimba,
kueleza sababu za kuwapo hati chafu Jiji la Mwanza ambako maelezo yao kwa
asilimia 90 yalifanana wakisingizia kupotea kwa nyaraka.
Sababu
nyingine ni zilizotolewa na watendaji hao ni kwamba Jiji la Mwanza lilipata
hati chafu kutokana na kukosekana ushirikiano kati ya wahasibu na wakaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu
za Serikali (CAG), kutokamilika miradi mingi ya maendeleo na wakurugenzi
kujichukulia uamuzi bila kushirikisha wahusika.
Kwa
upande wa maabara, hakuna wilaya hata moja ambayo itatimiza agizo la Rais la
kuwa na maabara ifikapo Novemba 30 mwaka huu kwa sababu majengo yapo kwenye boma
huku shule nyingine zikiwa hazijaanza ujenzi.
Sababu
zilizoelezwa kukwamisha shughuli hiyo ni baadhi ya viongozi wa siasa kuhamasisha
wananchi kutochangia, migogoro ya ardhi, ukosefu wa fedha na mambo mengine
mengi.
Kutokana
na maelezo hayo, Mulongo alisema anasikitishwa
kwa kitendo cha viongozi wa mkoa huo
kumdanganya kwa kumpatia taarifa ya maandishi
ambayo haina uwiano na maelezo yao na kuwaita kuwa ni viongozi mfilisi
walioagana na Serikali.
Mulongo alisema hataki kufanya kazi na
wakurugenzi wanaolalamikiwa na wananchi huku akuiwataka kuwatumia mgambo kama
chambo kwa wanachi, pia alikataa wananchi kunyang’anywa bidhaa zao huku akitoa
tahadhari kwa jeshi la polisi kutumiwa vibaya na viongozi kuhatarisha amani.
Maoni
Chapisha Maoni