Ray C: Ofa zilinivurugia ndoto zangu
MREMBO mwenye kujishughulisha na muziki wa Bongo
fleva nchini, Rehema ‘Chalamila ‘Ray C’, amedai kuwa ndoto zake za kuwa Dj mkubwa hapa nchini, zilivurugika baada ya kupata ofa ya kuimba na kurikodiwa wimbo
mmoja bure.
Awali kimwana huyo, aliwahi kuwa mtangazaji wa
kituo kimoja cha radio hapa nchini, alisema baada ya kurikodi wimbo huo,
mapokezi yake yalikuwa mazuri na hatimaye kuongezewa ofa ya albamu nzima bure
hali iliyomfanya asitishe kabisa utangazaji na kujitumbukiza katika ulimwengu
wa sanaa ya muziki wa bongo fleva.

“Nakumbuka
nilikuwa mtangazaji na DJ mzuri tu hapa nchini, lakini kutokana na kuwa na
kipaji kingine cha kuimba na watu walikitambua, ilinibidi nisitishe kitu kimoja
na kuegemea zaidi kwenye muziki kwasababu tayari mapokezi ya mashabiki yalikuwa
ni ya kutisha,”Ray C.
Anasema
anawaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kile anachookifanya, pia
yuko njiani kuachia ngoma mpya zitakazo rudisha heshima na hadhi yake ya
kipindi cha nyuma alichokuwa akishindanishwa na mkali wa bongo fleva Lady Jdee.
“Nakumbuka
enzi zangu nilikuwa nashindanishwa na wasanii wakubwa lakini sasa ushindani
umekuwa tofauti kabisa, nawaahidi mashabiki wangu wote kuwa letea burudai wanazozihitaji
ambazo zitarudisha ata heshima yangu katika hii sanaa,”
Maoni
Chapisha Maoni