Profesa Jay: Muziki wa sasa ni ajira si fani
MKONGWE wa Hip Hop nchini, Joseph Haule ‘Profesa J’ amekiri juu ya muziki wa
sasa kuwa ni ajira na si fani kama ilivyokuwa enzi zao miaka ya nyuma.
Mkongwe huyo
aliyetamba na wimbo wake wa ‘Nikusaidieje’ anasema muziki wa sasa unaonekana kuwa ajira kutokana na vijana wengi
kujitumbukiza katika tasni hii kwa ushindani wa hali ya juu huku kila mmoja
akijaribu kumvuta mwenzake ili yeye awe juu.

“Uanjua
kunautofauti mkubwa sana kati ya muziki wa sasa na waenzi zetu, ukizingatia
kila kukicha vijana wanaibuka katika muziki kama njia ya kujipatia ajira,
tofauti na miaka ya nyuma ambayo tulikuwa tunaimbia fani,”
Anasema,
hilo limeufanya muziki wa sasa kuonekana ni mwepesi wakati huo huo unaonekana
kuwa mgumu kutokana na chipukizi wenye vipaji na mitindo tofauti tofauti
wanayoibuka nayo kila kukicha kama ilivyo kwa Naseeb Abdul ‘Diamond Platnums’.
Maoni
Chapisha Maoni