Picha 10 za makabidhiano ya maktaba kati ya Shule ya Makumbusho na Read International

Displaying IMG_0151.JPGFaraja Kotta Nyalandu akikata utepe leo kwenye makabidhiano ya Maktaba kwenye shule ya Sekondari ya Makumbusho ya jijini Dar es salaam,kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Deogratias Haule,anaefata ni Afisa Elimu sekondari manispaa ya Kinondoni Omath Sanga na Mkurugenzi wa Read International Montse Penjuan, Maktaba hiyo imefadhiliwa na Shirika la Read International ambalo limenunu vitabu vyenye thamani ya fedha za kitanzania milioni 5,Kwa kushirikiana na International School of Tanganyika(IST) ya Dar es salaam ambayo wao wametengeneza mwonekano wa maktaba hiyo kama viti,meza na kabati.Displaying Library 1 .JPGMwonekano wa mbele wa maktaba hiyo kwa ndani mara  baada ya kukabidhiwa rasmi,kwa mkuu wa shule hiyo ya Makumbusho Deogratias Haule.Displaying IMG_0112.JPG
Upande wa pili wa maktaba hiyo.
Displaying IMG_0100.JPGMadaftari yatakayotumika kwaajili ya Kuweka kumbukumbu mbalimbali za Watumiaji wa Maktaba hiyo wanaokuja kuazima na kujisomea.Displaying IMG_0170.JPGFaraja Kotta ambaye pia anatarajia kuiunganisha shule hiyo na mfumo wa Shule Direct ambao yeye ndiye mwasisi siku chache zijazo, akiwa na wanafunzi watakaokuwa viongozi wa maktaba hiyo leo akiwaonsesha moja ya vitabu vyake.Displaying IMG_0182.JPGHapa Faraja Kotta akiwa kwenye picha ya pamoja na Gabo wa bongo movie na baadhi ya wanafunzi wa International School of Tanganyika waliotengeza maktaba hiyo pamoja nawatakao kuwa viongozi wa maktaba hiyoDisplaying IMG_0185.JPGGabo na Faraja wakifurahia jambo pamoja na wanafunzi hao.Displaying IMG_0192.JPGDisplaying IMG_0149.JPGFaraja Kotta akicheza muziki na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo kuonesha furaha yao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4